“Mtanipenda bado nikiimba at 50 ama mtanitroll?” – Nadia Mukami awauliza mashabiki wake

Muhtasari

• “Swali kwa mashabiki wangu: Mtanipenda bado nikiimba at 50?! 😁 ama mtanitroll 😁 mtasema oooh nipumzike,” Nadia aliwauliza.

Nadia Mukami
Nadia Mukami
Image: Instagram

 Mshindi wa tuzo ya Afrimma, Nadia Mukami ameshirikiana na msanii Masauti katika kibao kipya kwa jina ‘Kesho’ ambacho wanaulizana maswali mengi kuhusu maisha ya kesho.

Katika kibao hicho, Nadia mewakabili mashabiki wake na maswali mengi, akilenga kujua kama bado upendo walio nao kwake utadumu hadi pale atakapoamua kuimba akiwa na umri wa miaka 50 na Zaidi.

“Swali kwa mashabiki wangu: Mtanipenda bado nikiimba at 50?! 😁 ama mtanitroll 😁 mtasema oooh nipumzike,” Nadia aliwauliza.

Kwenye moja ya mistari yake kwenye wimbo huo, mama wa mtoto mmoja aliimba akisema kuwa anafahamu fika uzee upo, lakini atakata kujua kama mpenzi wake atamkubali baada ya uzee kumuingia na urembo kutoweka.

“Ninachojua uzee upo, usichana unakwenda, ule urembo haupo miaka ikienda, je utanipenda nikipata michirizi, utanipenda nikija nacho kitambi, nauliza utanipenda, yangu maziwa yakilala, uzeeni utanipenda, ama utaoa tena?” Nadia anauliza.

Kwa upande mwingine, Masauti ambaye aliwakilisha wanaume aliuliza maswali sawia,

“Kwanza ndio utanoga ukipata michirizi sio lazma flat tummy, nitacheza na kitambi, hivyo hivyo nitakupenda, hata kifua kija kulala, je name uzeeni utanipenda nikipata kihara?” Masauti aliuliza.