Marioo hajafurahishwa na cover ya albamu ya Willy Paul kisa rangi nyekundu ya ‘damu nyingi’

Kwa mujibu wa Marioo, muonekano huo wa nje ambao ni wa rangi nyekundu iliyokolea haujamvutia kwa vile kwake unazua dhana ya damu nyingi sana.

Muhtasari

• “Ngoma kali sana lakini hii cover iko na damu nyingi sana kakangu,” Marioo aliwambia Willy Paul.

WILLY PAUL
WILLY PAUL
Image: Instagram

Siku mbili baada ya Willy Paul kuachia rasmi albamu yake ya ‘Beyond Gifted’ – ambayo aliyoshirikisha wasanii wengi kutoka nje ya nchi, mmoja wa wasanii waliosjirikishwa kwenye albamu hiyo ameonekana kutovutiwa na rangi ya muonekano wa nje wa albamu hiyo.

Marioo, ambaye alishirikishwa na Willy Paul kwenye kibao cha ‘Nanana’ alitoa maoni yake kwenye ukurasa wa Instagram wa Willy Paul baada ya kuchapisha muonekano wa nje wa albamu yake na kolabo hiyo yao.

Kwa mujibu wa Marioo, muonekano huo wa nje ambao ni wa rangi nyekundu iliyokolea haujamvutia kwa vile kwake unazua dhana ya damu nyingi sana.

“Ngoma kali sana lakini hii cover iko na damu nyingi sana kakangu,” Marioo aliwambia Willy Paul.

Pozee aliwashangaza wengi kwa kutomjumuisha msanii wa Kenya hata mmoja katika ngoma 14 kwenye albamu hiyo.

Akijibu, Pozee alisema kuwa aliamua kutowashirikisha wasanii wa Kenya kwa kile alisema kuwa hawana lolote la kuchangia katika muziki Zaidi ya husda na chuki tu.

“Nimeona maswali mengi kuhusu ni kwa nini hakuna msanii hata mmoja wa Kenya kwenye albamu yangu. Kwani mumesahau kuwa wasanii wengi wa Kenya roho mbaya tu ndicho kitu wanamudu kwa bei nafuu? Albamu inatoka kesho mapema,” Willy Paul alisema.

Kando na ngoma zake binafsi kama Umeme, My child my love na Isabella, Willy Paul pia ameshirikiana na wasanii wa Bongo akiwemo Marioo, Nandy.

Pia kuna kolabo na wasanii wa Afrobeats kama Iyanya, Guchi, miongoni mwa wengine.