Lilian Nganga azungumzia alivyofaidika baada ya kufuta namba zote kwenye simu miaka 3 iliyopita

Takriban miaka mitatu iliyopita, mama huyo wa mvulana mmoja alitangaza kutengana na Alfred Mutua.

Muhtasari

•Lilian alisema kuwa simu yake sasa imejaa nambari za watu wapya ambao wanaathiri maisha yake vyema katika nafasi tofauti.

•Mke huyo wa mwimbaji Juliani alitumia tukio hilo kuwahimiza watu wasiogope kamwe kuanza upya.

Image: INSTAGRAM// LILIAN NGANGA

Lilian Nganga amefunguka kuhusu  jinsi alivyofanya uamuzi mgumu wa kufuta namba zote kwenye simu yake takribani miaka mitatu iliyopita.

Katika taarifa fupi kwenye mtandao wa Instagram, mama huyo wa mvulana mmoja alifichua kwamba uamuzi huo mgumu ulikuja na matokeo chanya.

Alisema kuwa simu yake sasa imejaa nambari za watu wapya ambao wanaathiri maisha yake vyema katika nafasi tofauti.

"Miaka 3 iliyopita, nilifuta nambari za watu kwenye simu yangu. Leo, simu yangu imejaa watu wapya wote wanaoniongeza katika maisha yangu katika nafasi tofauti,” Lilian Nganga alisema.

Mke huyo wa mwimbaji Juliani alitumia tukio hilo kuwahimiza watu wasiogope kamwe kuanza upya.

“Somo: Usiruhusu kamwe hofu itawale. Anza upya. Siku zote huchanua!” alisema.

Maisha ya Lilian Nganga yamepata mabadiliko mengi katika miaka mitatu iliyopita; amefunga ndoa na mwimbaji Julius Owino almaarufu Juliani, amemkaribisha mtoto wake wa kwanza, na hata amerejea kwenye kazi yake.

Takriban miaka mitatu iliyopita, mama huyo wa mvulana mmoja alitangaza kutengana na aliyekuwa gavana wa kaunti ya Machakos, Alfred Mutua.

Lilian na Mutua walitangaza kutengana kwao mnamo mwezi Agosti 2021  ingawa walikuwa wamekosana miezi miwili kabla ya kufichua hadharani.

Walipokuwa wanatangaza kutengana kwao, waziri Mutua aliahidi kuwa wangeendelea kuwa marafiki wazuri na kudai kuwa angeendelea kuomba Lilian ushauri.

Lilian hata hivyo baadaye alisema kwamba hapakuwa na uhusiano mzuri kati yake na Mutua tangu kutengana kwao, tofauti na madai ya waziri huyo wa utalii kwenye mitandao ya kijamii.

"Nilitamatisha uhusiano wangu na Alfred Mutua mwezi Juni mwakani(2021). Mara kadhaa haswa wiki katika kipindi cha wiki mbili zilizopita  nimeona Mutua akisema kwa gazeti na mitandaoni kuwa sisi ni marafiki na eti uhusiano wetu ulitamatika kufuatia maafikiano ya pamoja. Huo ni uongo wake wa kawaida. Hatujazungumza naye tangu mwishoni mwa mwezi Agosti. Lilian amesema.

Lilian alidai kwamba gavana Mutua alikuwa amekataa kabisa kusonga mbele na maisha yake licha ya mahusiano yao kufika kikomo.

Alidai kwamba Mutua aliathiriwa sana na kutengana huko na kufuatia hayo amekuwa akimpa vitisho pamoja na walio karibu naye.

Bwana Mutua ameguswa sana na kutengana kwetu. Ingawa nilisema nataka kusonga mbele na maisha yangu, alifikiria vingine" Lilian amesema.

Juliani na Lillian Ng'ang'a walifunga ndoa Februari 2022 na wanaonekana vizuri pamoja. Wawili hao walianza uchumba mara tu baada ya kutengana na Alfred Mutua.