Ugomvi kando! H-Baba ampongeza Diamond

Muhtasari

• H-Baba ameweka tofauti zao hizi pembeni kidogo na kumpa hongera stahili Platnumz kwa kuwa msanii wa kwanza tokea Masharii wa Afrika kutumbuiza katika hafla ya Grammy Global Spin.

• Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, H-Baba amempongeza Platnumz na kusema kwamba japo hamkubali lakini katika hili amemvulia kofia Pamoja na fulana.

H-Baba
Image: Instagram

Licha ya kutokuwa na uhusiano mzuri wa Sanaa baina ya msanii mkongwe wa miziki ya bongo fleva, H-Baba na msanii mwenzake Diamond Platnumz, H-Baba ameweka tofauti zao hizi pembeni kidogo na kumpa hongera stahili Platnumz kwa kuwa msanii wa kwanza tokea Masharii wa Afrika kutumbuiza katika hafla ya Grammy Global Spin.

H-Baba ambaye ana ukaribu na msanii Harmonize ambaye kwa siku za hivi karibuni amekuwa ni mbaya wake Platnumz, amempongeza msanii huyo kwa hatua hiyo kubwa ya kuheshimisha ukanda wac Afrika mashariki kwa ujumla, ukiachia mbali tofauti na beef za wanamziki wetu hao.

Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, H-Baba amempongeza Platnumz na kusema kwamba japo hamkubali lakini katika hili amemvulia kofia Pamoja na fulana.

Image: Instagram

“Mnyonge mnyongeni haki yake mpenii kwa Hili Umeuwaaaaaah JAPO SIKUKUBALI ILA KAMA NAANZA ANZA KUKUELEWA HIVI kwa Hili umeupiga Mwingi hongera @diamondplatnumz HII NI PAGE YANGU SIO YAKIKUNDI,” ameandika H-Baba.

Msanii Diamond aliandikisha rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kabisa kuwahi kutokea kutoka Afrika mashariki na kutumbuiza katika hafla ya Grammy, usiku wa kuamkia Februari 8 ambapo pia alizindua kibao chake kipya kwa jina #Gidi kwenye ukumbi huo.

Hongera sana Simba!