Stevo Simple boy na KRG The Don waridhiana

"Nilikusamehe baada ya kuona matatizo yote yanayokukabili," Krg alisema.

Muhtasari

•KRG The Don alimpa KSh5,000 taslimu na kuahidi kumuunga mkono katika shughuli zake za muziki.

•"Wakenya msupport Simple Boy mpaka anunue Prado kama hii"

Stevo na KRG
Stevo na KRG
Image: Facebook

Katika video iliyosambazwa na KRG, wawili hao walikuwa na gumzo ambapo rapper huyo alikiri kuwa hangekubali msamaha wa Stevo kama si hali ya kiuchumi inayomkabili kwa sasa.

"Nilikusamehe baada ya kuona matatizo yote yanayokukabili,"  Krg alisema.

Stevo alijitetea, akisema alinukuliwa vibaya na wakosoaji mtandaoni, na hakuwa na suala lolote na KRG The Don.

“Hii ni mambo ya mtandao. Mimi sina shida na wewe.”

Wakati akijieleza, Stevo alisema masaibu yake yanachangiwa na kutapeliwa na meneja wake wa zamani, lakini bahati yake ilikuwa karibu kubadilika baada ya kusajiliwa na Main Switch Group.

KRG The Don alimpa KSh5,000 taslimu na kuahidi kumuunga mkono katika shughuli zake za muziki.

"Kuanzia sasa na kuendelea tutakuwa tukifanya kazi na KRG The Don na kila kitu kingine kiko nyuma yetu sasa," Simple Boy aliyefurahi alisema.

Rapa huyo aliwataka Wakenya kuunga mkono talanta ya Simple Boy ili kumuinua kiuchumi.

“Wakenya msupport Simple Boy mpaka anunue Prado kama hii. Matapeli, wanawake, managers wamemuibia na nyinyi mnamsifu tu ati ako na talent. Kama mnajua ako na talent mnunue muziki, fresh barida juice na t-shirts mpaka anunue Prado.” Krg the don alisema.

Krg alijitolea  kumpeleleka Simple Boy nyumbani lakini mwanamuziki huyo alisema yuko  sawa.