Stevo Simple Boy aeleza kwa nini hapendi wimbo wake wa ‘Freshi Barida’

"Hizi nyimbo zingine mimi huwa sipendi. Haswa hizi Arbantone. Huo sio muziki, ni kuchachisha tu na nahisi uwepo wao utaisha tu haraka kama ambavyo Gengetone iliisha,” Simple Boy alisema

Muhtasari

• Stevo alieleza sababu ya kutopenda wimbo huo, akisema kuwa hakutiririka kwa mistari yake kama ambavyo alikuwa anataka, kwa hiyo kwake katika wimbo huo, alifanya chini ya wastani.

STEVO SIMPLE BOY.
STEVO SIMPLE BOY.
Image: Instagram

Msanii Stevo Simple Boy amefunguka kwamba katika nyimbo zake nyingi, moja ambayo hapendi kabisa ni ile ya ‘Freshi Barida’ ya mwaka 2022.

Katika mahojiano ya maswali ya haraka na Kenya Online Media, Simple Boy alieleza kwa mshangao wa wengi kwamba hapendi wimbo huo licha ya wengi kuhisi kwamba ndio wimbo ambao aliutendea haki katika mistari yake.

Stevo alieleza sababu ya kutopenda wimbo huo, akisema kuwa hakutiririka kwa mistari yake kama ambavyo alikuwa anataka, kwa hiyo kwake katika wimbo huo, alifanya chini ya wastani.

“Kwa ngoma zangu zote, moja ambayo ninapenda ni ‘Makasisi’ kwa sababu ni wimbo ambao unazungumza ukweli kuhusiana na wahubiri wa uongo. Na pia katika ngoma ambazo sipendi ni ‘Freshi Barida’, siku’flow vile nilikuwa nataka. Hata kama mashabiki wengi wanaupenda huo wimbo, lakini kutoka kwangu kama mtunzi, siupendi,” Stevo alisema.

Rapa huyo alisema kwamba nchini Kenya kama kuna msanii ambaye anamtambua kabisa ni rapa mwenza, Khaligraph Jones, lakini akafichua kwamab angependa sana kufanya kolabo na Nadia Mukami.

“Kwa Sanaa ya Kenya msanii ambaye napenda ni Khaligraph Jones, ni msanii wa hiphop kama mimi, ako na flow na mistari, hizi nyimbo zingine mimi huwa sipendi. Haswa hizi Arbantone. Huo sio muziki, ni kuchachisha tu na nahisi uwepo wao utaisha tu haraka kama ambavyo Gengetone iliisha,” Simple Boy alisema.