Stevo Simple Boy adai mamilioni kurudiana na Pritty Vishy, kumuoa na​​kumpachika mimba

Mtunzi huyo wa kibao wa ‘Freshi Barida’ alibainisha kuwa tayari amepanda bei.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo kutoka Kibera aliibua malalamiko kadhaa wakali dhidi ya mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22.

•Pia alizungumza juu ya uwezekano wa kufufua uhusiano wao uliovunjika ambapo alitoa masharti mazito ili hilo kutokea.

Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Stivo Simple Boy na aliyekuwa mpenzi wake Pritty Vishy
Image: SCREENGRAB// MUNGAI EVE

Rapa maarufu wa Kenya Stephen Odero almaarufu Stevo Simple Boy ameweka wazi kuwa yeye ha’miss chochote kuhusu mpenzi wake wa zamani Pritty Vishy.

Akiongea kwenye mazungumzo na Eve Nyaga, mwimbaji huyo kutoka Kibera aliibua malalamiko kadhaa wakali dhidi ya mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22.

Pia alizungumza juu ya uwezekano wa kufufua uhusiano wao uliovunjika ambapo alitoa masharti mazito ili hilo kutokea.

“Kwanza, kuomba msamaha anafaa atoe elfu hamsini, akitaka turudiane alete laki tano, na akitaka nimpachike mimba alete milioni moja, na akitaka tufanye harusi milioni mbili,” Stevo alisema.

Mtunzi huyo wa kibao wa ‘Freshi Barida’ alibainisha kuwa tayari amepanda bei.

Vishy alitengana na Simple Boy mapema mwaka wa 2022, miezi michache tu baada ya mahusiano yao kujulikana hadharani.

Wawili hao hata hivyo ilidaiwa hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwani Stevo Simple Boy alidaiwa kutaka kusubiri ndoa kabla ya kushiriki tendo la ndoa na mtumbuizaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

Katika mahojiano ya mwaka jana, Stivo alidokeza kwamba alichumbiana na Pritty Vishy wakati bado akiwa na mke wake, Grace Atieno. Alisema alipima tabia za wawili hao kabla ya kuamua mke wa kuwa naye. 

"Ukiwa na wasichana wawili unaangalia ni nani ako na utu, na ni nani ako wema na unyenyekevu. Kwangu mimi, unyenyekevu na kuvumilia kwake zilifanya nikavutiwa kwake," alisema msanii huyo kutoka mtaa wa Kibera.

Mwaka uliopita, Pritty Vishy alikuwa amedokeza kuwa kwenye mahusiano na mcheza santuri, DJ Starvy. Baadaye hata hivyo ilibainika kuwa wawili hao walikuwa wanataniana tu na hawakuwa wapenzi.