Weezdom amtambulisha mpenzi mpya kwa wanamitandao

Muhtasari

•Baada ya kutangaza  kuachana na  Mylee  Staicey, Weezdom  ametambulisha rasmi  mpenzi wake  mpya kwenye mitandao yake ya  kijamii.

•Hii imewadia  siku chache baada ya  Weezdom kuonya aliyekuwa mpenzi wake, Mylee kukoma kutumia jina lake kwenye mahojiano na wanahabari

 

Weezdom na mpenzi wake mpya
Weezdom na mpenzi wake mpya
Image: instagram/weezdom

Baada ya kutangaza  kuachana na  Mylee  Staicey, Weezdom  ametambulisha rasmi  mpenzi wake  mpya kwenye mitandao yake ya  kijamii.

Hii imewadia  siku chache baada ya  Weezdom kuonya aliyekuwa mpenzi wake, Mylee kukoma kutumia jina lake kwenye mahojiano na wanahabari.

“Mwambieni Mylee Staicey kuwa Mungu alinipa uwezo wa kumjua. Na mimi niko na ushahidi wa kila kitu kuhusu mahusiano yangu na yeye , hivyo  aache kutumia jina langu kutengeza kiki, sitaki tuaibishane,” alisema Weezdom

Wiki hii, amepakia picha kwenye ukurusa wa instagram, picha ambayo ilikuwa inaonyesha wapenzi hao wawili.

Mashabiki wametumia  sehemu ya maoni kumtania kwa kasi aliyoingia kwenye mahusiano mengine.

@scolasticakivina-haraka ajee

 @muthoni__mugo- Unasonga kuliko boda mtu wangu@ djeuphorique-Sawa kaka  mimi nimejitoa  kuwa wewe ni ndugu yangu kabisaaaa