Niliamua kufanya kinyume; mtoto kwanza, ndoa baadae - Jacky Vike

Muhtasari

• Muigizaji na mwanamuziki Jacky Vike amesema kwamba yeye aliamua kufanya kila kitu kinyume na matarajio ya jamii.

• Aliamua kuanza kupata mtoto na mambo mengine katika taratibu za mila kufuata baadae

Jacky Vike Awinja
Image: Facebook

Muigizaji na mwanamuziki Jacky Vike amesema kwamba yeye aliamua kufanya kila kitu kinyume na matarajio ya jamii na hana lolote la kujutia maamuzi yake hayo ya kufanya mambo yake tofauti na kawaida.

Muigizaji huyo alifichua kwamba alifanya maamuzi ya kupata mtoto kwanza ndio mambo mengine ya ndoa na taratibu za mila zifuate baadae, kinyume na ilivyo katika jamii nyingi za Kiafrika ambapo wengi wanataka ndoa kwanza halafu mipango ya kupata watoto inafuata.

“Sisi ni watu ambao tumefanyqa maamuzi ya kufanya vitu tofauti na kinyume na wengi. Najua wengi wanasema kwamba kuchumbiana kunafaa kuja kwanza, halafu kulipa mahari, kuoana na kisha kupata mtoto. Lakini mimi nilichagua kufanya kila kitu kinyume na taratibu hizo na naona kila kitu kinaenda shwari na mimi. Sina haraka mimi, na kusema kweli napenda hivi,” alisema Awinja.

Akizungumza katika mahojiano ya kipekee na SPM Buzz, Awinja alisema kwamba hajutii kupata mtoto na pia akasema mzazi mweziwe wanashirikiana vizuri katika malezi ya mwanao na wako na maelewano mazuri sana.

“Baba mtoto yuko tena sana katika Maisha na mwanetu. Tulianzia mwisho kurudi nyuma lakini kila kitu kitatupata mbele. Nilikuwa tayari kuwa na mtoto kwa sababu tumekuwqa katika mahusiano kwa muda mrefu Zaidi,” alisema Awinja.