Diana B amenisurprise, namkubali sana - Weezdom

Muhtasari

• Msanii Weezdom ameweka bayana kwamba anamkubali mwanamuziki chipukia, Diana B ambaye ameachia ngoma yake ya #mubaba siku chache zilizopita na inazidi kufanya vizur katika mtandao wa YouTube na kwenye chati mbalimbali za muziki.

• Akizungumza na mwanablogu Nicholas Kioko, Weezdom amesema kwamba Diana Marua amemshangaza kutokana na ukomavu wa mashairi yake ambayo yameonekana kukaririwa sana na kwa wepesi na mashabiki wake

Msanii Weezdom ameweka bayana kwamba anamkubali mwanamuziki chipukia, Diana B ambaye ameachia ngoma yake ya #mubaba siku chache zilizopita na inazidi kufanya vizur katika mtandao wa YouTube na kwenye chati mbalimbali za muziki.

Akizungumza na mwanablogu Nicholas Kioko, Weezdom amesema kwamba Diana Marua amemshangaza kutokana na ukomavu wa mashairi yake ambayo yameonekana kukaririwa sana na kwa wepesi na mashabiki wake.

Aidha Weezdom ameongeza kwamba kipindi alikuwa chini ya lebo ya EMB, Diana hakuonyesha dalili yoyote ya kuingia kwenye muziki na wala hangeweza kuandika hata shairi moja, jambo ambalo linasababisha yeye kumkubali zaidi kwa hatua ambazo amezipiga.

Kutokana na tofauti ambazo zimekuwepo kwa muda mrefu baina ya Weezdom na Bahati ambaye ni mumewe Diana B, wengi walitarajia kwamba hangemuunga mkono ila Weezdom ameonyesha ukomavu na kukubali ngoma zake kwa sana.

Kuhusu usanii wake, Weezdom amesema kwamba aligura sekta ya miziki ya injili ila uhusiano wake na Mungu bado upo imara. Ameongezea kwamba akitaka kuimba ataingia studioni wakati wowote na kutoa kazi ambayo anajua itamfurahisha Mungu.