Sitaki kuwa na chuki na mtu,sina chuki na msanii yeyote-Weezdom afunguka

Muhtasari
  • Weezdom aweka wazi hana ugomvi na msanii yeyote
  • HUku akizungumzia kibao cha Bahati cha 'Fikra za Bahati' alisema kuwa hakupenda kibao hicho kuanzia mwanzoni

Msanii Weezdom akiwa kwenye mahojiano na  runinga ya Switch alifunguka jinsi alitoka kwenye kampuni ya msanii Bahati.

HUku akizungumzia kibao cha Bahati cha 'Fikra za Bahati' alisema kuwa hakupenda kibao hicho kuanzia mwanzoni.

"Nilikuwa katika timu ambayo ilikuwa inazindua albamu ya Bahati lakini nikatoka, sikupenda kibao cha Bahai lakini nampenda sana

Namshukuru Bahati kwa kuniamini kama msanii, sina chuki na msanii yeyote, na wala sitaki kuwa na chuki kwani nataka amani itembee

Sioni nikirudi kwenye tasnia ya usanii lakini nataka kuzindua shirika langu," Aliesma Weezdom.

Huku akizungumzia ugomvi wake na msanii Peter Blessings alisema haya.

"Nilisamehe kila mtu sina chuki, wala ugomvi na Blessings lakini angekaa na msanii Bahati angekuwa mbali

Wapenzi wangu wa kitambo ni marafiki zangu, nina baby mama 3 na mpenzi wangu anawajua,"