Mpenzi wa Weezdom, Stacey Ndaisi ajitosa kwenye siasa

Muhtasari

• Mylee Stacey Ndaisi, ambaye ni mpenzi wa msanii wa injili Weezdom ametangaza kujibwqaga kwenye ulingo wa siasa.

• Akiweka kwenye ukurasa wake wa Instagrqam, Ndaisi ametangaza kuwqania ubunge wa Kibwezi Magharibi kwa chama cha ODM.

Stacey Ndaisi
Image: Stacey Ndaisi (Instagram)

Mylee Stacey Ndaisi, ambaye ni mpenzi wa msanii wa injili Weezdom ametangaza kujibwqaga kwenye ulingo wa siasa.

Akiweka kwenye ukurasa wake wa Instagrqam, Ndaisi ametangaza kuwqania ubunge wa Kibwezi Magharibi kwa chama cha ODM.

Awali, Ndaisi alikuwa amewatangazia wafuasi wake kwamba alikuwa na tangazo kubwa maalum Januari 31 kwanzia saa nne asubuhi, na wengi wa wafuasi wake walikuwa ange kusikia ni tangazo lipi angesema huku akiwatania kwamba mwenye atatabiri kweli kuhusu tangazo lake angejishindia mjazo wa simu wenye thamani ya shilingi elfu moja.

Image: Stacey Ndaisi (Instagram)

Katika Tangazo hilo, Ndaisi alisema watu wa eneo bunge la Kibwezi Magharibi kilio chao cha muda mrefu kimesikika na yupo tayari kuyamaliza matatizo yao kabisa.

"Watu wa eneo bunge la Kibwezi Magharibi, kilio chenu kimesikika. Nipo tayari kabisa kuwahudumia kama mbunge wenu mwaka 2022. Pamoja Tubadilishe KIBWEZI. Fom Ni Azimio La Umoja Na Msisahau Kuchukua Kura Watu Wangu," alifuatisha ujumbe huu na bango la picha yake lenye rangi za muungano wa Azimio La Umoja.

Wengi wa mashabiki wake wamefurika mitandaoni kumpa hongera na kumtakia kila la kheri katika azma yake ya kuwahudumia watu wa Kibwezi Magharibi kama mbunge.