Weezdom amlaumu Bahati kwa 'views' zake kupotea YouTube

Muhtasari

• Kulingana na Weezdom, Views za ngoma yake mpya ' Wazae' ziliporomoka kutoka laki moja hadi elfu tatu chini ya saa ishirini na nne, na anasema Bahati yuko nyuma ya njama hiyo ya kumdidimiza kimuziki.

Weezdom, Bahati
Image: Facebook

Aliyekuwa msanii wa injili Weezdom amezua mapya baada ya kudai kwamba Bahati ako nyuma ya kumdidimiza kimuziki na kusema kwamba Bahati ndiye alipanga njama ya kupunguza ‘views’ za ngoma yake mpya ya ‘Wazae’ kutoka elfu mia moja hadi elfu tatu chini ya saa ishirini na nne kwa kile kinatajwa kwamba ni mzozo wa kuibiwa kwa mawazo ngoma ya Diana B.

Akizungumza katika kituo kimoja cha redio humu nchini wakati wa ‘Media tour’ yake akiitambulisha collabo hiyo yake na Manzi wa TRM baada ya kimya cha muda mrefu, Weezdom alisema kwamba mpaka amelifuatilia suala hilo la kupotea kwa ‘views’ za ngoma yake kwa wasimamizi wa mtandao wa YouTube nchini Afrika Kusini na ana uhakika wa kile anachokisema kwamba Bahati ndiye anafanya njama hiyo.

 “Mimi sikununua views lakini kuna ndugu yangu ambaye anajaribu kuni-sabotage kwa YouTube, na nasema hili kwa sababu nimefuatilia mpaka kwa watu wa YouTube South Africa. Analipia kuniharibia ili nionekane sina watu wengi wanaonifuatilia YouTube lakini tutafix,” alisema Weezdom.

Msanii huyo pia alisema kwamba hasemi hivo kwa sababu ya kutafuta kiki bali ni ukweli kwamba ngoma hiyo watu waliona ilifika ‘views’ laki moja na baadae zikashuka hadi elfu tatu. Akiulizwa ndugu yake huyo ni nani, Weezdom alisita kwa muda lakini mwisho wa siku akafunguka na kumtaja kwa jina.

“Mimi naeza omba tu Bahati aniruhusu mimi niendelee kuimba, yaani isiwe kwa sababu mimi sina pesa kama yeye, isiwe kama tunashindana,” alitema nyongo Weezdom.

Msanii huyo pia alisema kwamba si kumsingizia Bahati kwa sababu ni kweli na kama Bahati atahisi kwamba anasingiziwa basi ni bora achukue hatua za kisheria kwani ukweli wote Weezdom anao.

Kwa upande wake Manzi wa TRM alisema kwamba mpaka wako na barua pepe ambayo ilitumiwa mtu wa karibu nao ikisema kwamba katika ngoma yao ya ‘Wazae’ waliimba mawazo ya ngoma ya mke wa Bahati, Diana B ya ‘Mubaba’ na hicho ndicho chanzo kikubwa cha mwanzo wa vita vyao.

Aidha Weezdom amesisitiza kwamba hana shida na Bahati kwa sababu anamkubali kuwa mtu mwenye bidii lakini pia ni bora Bahati amuache na yeye akazane na muziki.