Je kibao cha Diana Marua cha 'Mubaba' kinachangia usherati katika jamii na kizazi cha sasa?

Muhtasari
  • Diana hakuwasikiza wote ambao walimkejeli bali aliendelea kuachilia kibao kimoja baada ya kingine
  • Wiki iliyopita msanii huyo alitoa kibao ambacho kinafahamika kama 'Mubaba'
Diana Marua
Diana Marua
Image: hisani

Diana Marua alijitosa kwenye tasnia ya muziki mwaka jana, huku akijiita kwa jina Diana B, kujitosa kwake kulipokea hisia tofauti mitandaoni huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza huku wengine wakimkejeli.

Diana hakuwasikiza wote ambao walimkejeli bali aliendelea kuachilia kibao kimoja baada ya kingine.

Wiki iliyopita msanii huyo alitoa kibao ambacho kinafahamika kama 'Mubaba'.

Ni kibao ambacho kinazungumzia hali ya sasa na jinsi kizazi cha sasa kinajigamba hasa wanawake wanapoanza tabia ya kupata 'sponsor'.

KIlipokelewa na hisia tofauti na wakenya, huku baadhi yao wakisema na kudai kwamba kinachangia ushereti katika jamii.

Ndio vijana wengi wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanazungumziwa kwenye kibao hicho,lakini badala ya kuwakashifu kibao chake Diana kinawashauri jinsi ya kufanya mambo haya.

Je kulingana na maoni yako, kibao chake Diana kinachangia usherati katika jamii zetu na kizazi cha sasa?