Nataka mwengine mmoja tu, Bahati amwambia Diana Marua

Muhtasari

• Msanii Bahati amekiri kwamba angependa kupata mtoto mmoja na wa mwisho.

• Hii ni kupitia video iliyoachiwa katika mtandao wa YouTube wawili hawa wakionekana kuwa katika majibishano huku Diana amabaye ni mke wake akidai kwamba walipaswa kuelewana kuhusu jambo hilo lakini baadaye alikubali kuwa angemzalia Bahati mtoto wakati wowote akiwa tayari.

Image: INSTAGRAM//DIANA MARUA

Msanii Bahati amekiri kwamba angependa kupata mtoto mmoja na wa mwisho.

Hii ni kupitia video iliyoachiwa katika mtandao wa YouTube wawili hawa wakionekana kuwa katika majibishano huku Diana amabaye ni mke wake akidai kwamba walipaswa kuelewana kuhusu jambo hilo lakini baadaye alikubali kuwa angemzalia Bahati mtoto wakati wowote akiwa tayari.

“Mimi niko na promise ama sijui ni request moja, nataka tu unipe motto mwengine mmoja tu,”alisema Bahati.

Bahati akionekana kuwa mwenye furaha nyingi kutokana na jibu hilo la mkewe, aliahidi kuwa atafanya harusi kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa humu nchini na pia atazidisha penzi lake kwake na kwa watoto wao ili kulea familia yenye upendo.

Kwa upande wake Diana Marua, alimshukuru mumewe kwa kuhakikisha anafanya kila awezalo kuona kwamba anazidi kunawiri katika jambo lolote analolifanya, la hivi majuzi likiwa kumpa sapoti katika hatua yake ya kuingia kwenye muziki. Ameahidi kumpenda daima na kulea watoto wao kwa misingi komavu ambayo itawajengea kesho yao ambayo itakuwa bora zaidi.

Wawili hawa ni moja kati ya watu maarufu humu nchini ambao ndoa zao zimesimama kwa muda mrefu na ambao pia wanapiga hatua nyingi na kubwa katika sanaa, huku wakiwamotisha vijana wengi ambao wangependa kufuata nyayo zao.

La mno ambalo litakuw linasubiriwa kwa sasa ni harusi kubwa aliyoisema Bahati japo hakutaja mwaka na tarehe ambapo hafla hiyo itafanyika.