'Nakufa,nahitaji msaada,'Johnstone Letoya asema huku akiweka wazi ana msongo wa mawazo

Muhtasari
  • Kulingana na chapisho alilochapisha katika ukurasa wake wa instagram Letoya hajui jinsi anavyoishi
Letoya Johnstone
Image: Radiojambo

Mtetezi wa haki za kibinadamu Letoya Johnstone ambaye alizaliwa akiwa na jinsia ya uume 'Transgender' amewaacha wanamitandao wakimtakia kila la heri baada ya kufichua kwamba ana msongo wa mawazo.

Kulingana na chapisho alilochapisha katika ukurasa wake wa instagram Letoya hajui jinsi anavyoishi.

Pia mtetezi huyo alisema kwamba ni inadamu ambaye yuko mpweke kwani marafiki wake walimkimbia.

"Moyoni mwangu ninaugua msongo wa mawazo! Kuna mambo ambayo marafiki wa zamani waliniwekea na kila siku naamka najifungua.

Sijui ninaishije katika hili lakini tutegemee watu watalazimika kuandika pumziko kwa amani.

Mimi ndiye binadamu mpweke zaidi nikiwa hai bila rafiki hata mmoja. Wageni ambao hawakuwahi kukutana nami wananifanyia kilicho bora zaidi. Asante sana ❤️

Angalia hadithi ya Jonny Depp au hadithi ya Robin Williams.Watu mashuhuri kama sisi wanapitia mambo yasiyowazika lakini lazima tuunde uso huu ili kuwafanya wengine waone kung'aa ndani yetu. Hiyo ndiyo kila mtu huvutiwa nayo.

NAHITAJI MSAADA WATU WANGU..... NAKUFA. Tafadhali nisaidie 😭,"Aliandika Letoya.