Napenda watoto sana, lakini naona nikilea wa wenyewe-Mcheshi Nasra Yusuf

Hata hivyo Nasra amesema kwamba anaona akiwalea watoto wa mtu mwingine au amruhusu mumewe aoe bibi wa pili.

Muhtasari
  • Mchekeshaji huyo pia aliandika kwamba amepoteza zawadi yake kabla hata ya kuipokea mikononi licha ya kuweka maandalizi mazuri

Siku chache baada ya kutangaza kifo cha mtoto wao mchekeshaji wa Churchill Show Nasra Yusuf amesema kwamba anapenda watoto sana.

Kupitia kwenye kipindi cha Q&A cha instagram mchekeshaji huyo alikuwa anamjibu mmoja wa mashabiki wake aliyeuliza iwapo atapata watoto wengine katika maisha yake ya usoni.

Hata hivyo Nasra amesema kwamba anaona akiwalea watoto wa mtu mwingine au amruhusu mumewe aoe bibi wa pili.

"Ungependa kupata watoto katika maisha yako ya usoni,"Shabiki aliuliza.

"Napenda watoto sanaaa lakini Wueh naona nikilea wa wenyewe sasa..ama nikubali Director aoe mke wa pili," Alijibu Nasra.

Huku akitangaza habari za kumpoteza mwanawe,Mchekeshaji huyo pia aliandika kwamba amepoteza zawadi yake kabla hata ya kuipokea mikononi licha ya kuweka maandalizi mazuri kutoka jina, nguo na kila kitu kinachohitajika katika maandalizi ya kumpokea mtoto anapozaliwa.

β€œKumpoteza malaika wangu mdogo kabla hata sijakutana naye hufanya iwe vigumu zaidi kuamini πŸ’”πŸ’”Nilifurahia sana safari hii, nilikuwa na kila kitu, kuanzia jina, hadi aina ya maisha ambayo angefikiria akilini mwangu..ooh natamani kuuona uso wako tu mtoto wanguπŸ’™πŸ’“lakini ALHAMDHULILAH,” Nasra Yusuf aliomboleza.

Yusuf aliomboleza kifo cha kijusi chake na kusema kwamba haamini amefariki lakini pia akashukuru kwa kusema kuwa huenda huyo ndiye atakayekuwa bahati yake ya kuingia peponi.