Madonna, 64, afichua siri ya kuwa mbichi muda wote, "Kushiriki tendo la ndoa kila mara" (+video)

Alikuwa akijibu maswali 50 kwenye YouTube yake.

Muhtasari

• Msanii huyo pia alisema kwamba maamuzi ambayo aliwahi kuyafanya na kujutia sana mpaka kutaka kurudisha muda nyuma ili kurekebisha ni pale alipokubali kuolewa.

• Madonna aliolewa na Sean Penn kutoka 1985 hadi 1989, na baadaye alifunga ndoa na Guy Ritchie mnamo 2000, kabla ya kutengana mnamo 2008.

Staa wa muziki aina ya pop kutoka Marekani, mwanamama Madonna mwenye umri wa miaka 64 hatimaye amefichua siri ya kuzidi kubaki mbichi licha ya umri wake kusonga mbele kweli kweli.

Akijibu maswali ya mashabiki wake kupitia kipondi kifupi cha maswali na majibu kwenye ukurasa wake wa YouTube, Madonna aliulizwa maswali mbali mbali ambayo alipata kuyajibu pasi na kuogopa.

Wengi walionekana kutaka kujua siri ya urembo wake licha ya umri wa kizee na wengine maswali mengi tu ambayo yalizunguka safari yake ya muziki na maisha ya familia na ndoa mbii zilizosambaratika.

Majibu yake mengi yaliwashangaza mashabiki wake ambapo kila kitu alikuwa anajibu kwamba ni kutokana na kushiriki ngono.

Katika moja ya swali, aliulizwa ni kitu kipi haramu ambapo amewahi kukifanya na kikampa Faraja tele moyoni ambapo alijibu kwamab ni kushiriki tendo la ndoa.

Pia alisema kwamba siri ya urembo wake pamoja na kung’ara kwa Ngozi yake licha ya kuwa na umri mkubwa, Madonna alijibu kwamba siri ni kushiriki ngono kila mara.

Msanii huyo pia alisema kwamba maamuzi ambayo aliwahi kuyafanya na kujutia sana mpaka kutaka kurudisha muda nyuma ili kurekebisha ni pale alipokubali kuolewa.

Kwa wale wafuatiliaji wa historia ya mwanamuziki huyu mkongwe, myakumbuka kwamba aliolewa na Sean Penn kutoka 1985 hadi 1989, na baadaye alifunga ndoa na Guy Ritchie mnamo 2000, kabla ya kutengana mnamo 2008.

Madona alijibu maswali hamsini kwa haraka chini ya dakika sita kwenye video hiyo ambayo unaweza ukaitizama hapo juu.