Nikifa Alikiba asifike kwa msiba wangu, Diamond anizike ili nife kwa furaha - Issa Azam

Msimamizi wa msiba wangu atakuwa Naseeb Abdul - Issa Azam.

Muhtasari

• Alisema Diamond anamlipa mshahara mara 4 ya mbunge.

• "Alikiba asifike kabisa kweney msiba wangu, hata kwangu aijaribu kufika,” Issa Azam alisema.

Chawa wa Diamond alisema kwamba yupo radhi kumukoa Diamond kutoka motoni na kuiacha familia yake
ISSA AZAM, DIAMOND na ALIKIBA Chawa wa Diamond alisema kwamba yupo radhi kumukoa Diamond kutoka motoni na kuiacha familia yake
Image: Instagram

Issa Azam, ndugu wa toka nitoke wa msanii Alikiba ambaye alifanyakufuru ya karne kumtenga nduguye na kuungana na mbaya wake Diamond Platnumz ameibuka na mapya tena.

Mjasiriamali huyo mwenye ukaribu sana na msanii Diamond Platnumz wengi wanamjua kama chawa wa WCB Wasafi.

Issa mwenyewe mara kadhaa amekuwa akiliweka wazi suala hilo na sasa amezungumzia mshahara anaoupata kutoka kwa Diamond Platnumz kwa kazi yake ya uchawa.

Issa kwa kuwakomesha wanaomsema vibaya simba, mshahara wake alisema ni mnono sana kwac mwezi.

Akizungumza na kituo cha Wasafi katika kipindi cha Refresh, Issa Azam alifunguka kwamba mshahara wake kutoka kwa bosi Diamond Platnumz ni mara nne zaidi ya mbunge.

“Mimi mshahara yangu nikiungaunga, ni mshahara minne ya mbunge,” Issa alisema tena kwa mikogo.

Alizidi kuendeleza chuki yake dhidi ya Alikiba na wanafamilia wengine kwa kile alisema kwamba aliwachukia kwa kutaka kumuua Diamond kwa kumpiga mawe ila wakashindwa.

Issa aliweka wazi kwa mara nyingine tena kwamba ikitokea amefariki leo hii basi watu wa familia ya Alikiba wasijaribu kufika kweney msiba wake kumzika.

“Mimi leo hii nikifa, kwenye kaburi langu nisiwahi waona watu hao. Msiba wangu utasimamiwa na watu wa Wasafi. Msimamizi wa msiba wangu atakuwa Naseeb Abdul (Diamond Platnumz). Naomba Diamond anizike ili nife kwa furaha. Alikiba asifike kabisa kweney msiba wangu, hata kwangu aijaribu kufika,” Issa Azam alisema.