Bien ataka Wizara ya Michezo kutengenishwa na ya Utamaduni

Wizara ya vijana, michezo, utamaduni ilipewa Ababu Namwamba.

Muhtasari

•Mwimbaji huyo amesema sekta ya utamaduni inafaa kuwa na wizara yake pekee na sio kuunganishwa na ya michezo.

•Haya yanajiri baada ya rais William Ruto kutangaza baraza lake la mawaziri jana  siku ya Jumanne.

Bienaimesol
Image: Bien Instagram

Mwanamuziki wa kikundi cha Sauti Sol, Bien Aime Baraza almaarufu Bien Sol ametoa maoni yake kupitia ukurasa wake wa Instagram kuhusu mawaziri wapya walioteuliwa na rais William Ruto mnamo Jumanne.

Bien alizungumza kuhusu wizara ya michezo na kitamaduni ambalo huleta pamoja sekta mbili tofauti za burudani.

Mwimbaji huyo amesema sekta ya utamaduni inafaa kuwa na wizara yake pekee na sio kuunganishwa na ya michezo.

Alieleza kuwa michezo na utamaduni ni nyanja mbili tofauti ambazo hazifai kuwa chini ya wizara mmoja.

“Wizara ya utamaduni unafaa kuwa na ofisi yake peke yake kado na ya michezo. Michezo na utamaduni ni mambo mawili tofauti,”alisema.

Pia alisema kuwa mataifa yenye umakini yamezingatia utamaduni. Alisema mataifa hayo yametenganisha wizara ya utamaduni na wizara yoyote nyingine ile.

"Patieni mambo haya mawili nguvu sawa,”mwanamuziki huyo alisema.

Haya yanajiri baada ya rais William Ruto kutangaza baraza lake la mawaziri jana  siku ya Jumanne.

Wizara ya vijana, michezo, utamaduni ilipewa aliyekuwa katibu mkuu katika wizara ya mambo ya nje Ababu Namwamba.

 Ababu ambaye aliwahi kuhudumu tena katika wizara ya michezo alichangia katika kupitishwa kwa Sheria ya Michezo mwaka wa 2013.

Sasa ambapo Namwamba amepewa fursa hiyo ataweza kuendelea na kazi yake aliyokuwa ameanzisha.

Namwamba ametarajiwa kuleta matumani kwenye sekta ya michezo hasa sasa ambapo ligi kuu ya Kenya imeweza kurejea.