Pole Masanja, ila vijana oeni wanawake wasio na tamaa za kijinga - Mwijaku

Vijana oeni wanawake wasio na tamaa za kijinga kushiriki mapenzi na kila mtu kizembe - Mwijaku.

Muhtasari

• Mwijaku alimpa pole mchungaji Masanja Mkandamizaji kwa skendo inayomhusisha mkewe kimapenzi na katibu wa kanisa aliyejiua.

Mwijaku ampa pole Masanja Mkandamizaji
Mwijaku ampa pole Masanja Mkandamizaji
Image: Instagram

Baada ya sakata la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa la Feel Free lake mchekeshaji ambaye sasa ni mhubiri Masanja Mkandamizaji, sasa watu wengi wamezamia skendo hiyo na kutolea maoni mseto.

Ikumbukwe zogo zima la katibu huyo kujitoa uhai liligeuka changamano hata zaidi baada yake kuacha barua ambayo alimuandikia mkewe mchungaji Masanja Mkandamizaji na kudhihirisha kwamba anampenda sana na yeye alikuwa analijua hilo na ndio maana wivu wa mapenzi umemfanya kujisafirisha jongomeo.

Baada ya tarifa hizo za mkewe baba mchungaji kutoka kimapenzi na mama kanisa, Masanja alizungumzia suala hilo na kuahidi kuzidi kumpenda mkewe hadi pumzi zake za mwisho licha ya skendo ya kimapenzi na marehemu katibu wa kanisa lao.

Mtangazaji Mwijaku pia hajaachwa nyuma kwani amelizamia na kumwambia Mchungaji pole za dhati kwa matukio yanayozunguka kanisa lake pamoja pia na mke wake kutoka kimapenzi na katibu wa kanisa.

Mwijaku ametumia fursa hiyo kutoa onyo kali kwa watu watakaojaribu kufanya mzaha wa kumtongoza mkewe kuwa atawapiga bomu vibaya sana.

Pia aliwashauri vijana kuoa wanawake wasiokuwa na tamaa za kijinga kama mkewe katika kile kilionekana anamkashfu mke wa Masanja kwa kuhusishwa kimapenzi na katibu wa kanisa lake.

“Pole Masanja, Nawakumbusha vijana oeni wanawake wenye ustaamilivu na uvumilivu kama mke wangu, asiye na tamaa za kijinga za kushiriki mapenzi kizembe,” Mwijaku alishauri.

“Sema nawaonya mie mtu akinichezea kwenye utamu wangu hata kama anajiua yaani mimi namfufua na kumuua tena na nimfilimbe ndio azikwe,” aliongeza kwa kutoa onyo.