Hatimaye Kimani Mbugua aondoka kutoka hospitali ya kiakili ya Mathare

Hili linajili baada ya Mbugua kudai kwamba alikuwa amezuiliwa kwenye hospitali ya Mathare kinyume na matakwa yake.

Muhtasari

• Mbugua huku akishukuru alisema hatimaye yupo nyumbani kwa wazazi wake huko Murang'a.

• Mbugua aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter akiomba wanamitandao kuwashinikiza wazazi wake kumtoa katika hospitali hiyo.

Aliyekuwa mtangazaji wa Citizen TV Kimani Mbugua
Kimani Mbugua Aliyekuwa mtangazaji wa Citizen TV Kimani Mbugua
Image: Instagram

Aliyekuwa mtangazaji wa runinga Kimani Mbugua sasa amerejea nyumbani kwa wazazi wake baada ya kudai kwamba alikuwa amezuiliwa kwenye hospitali ya Mathare kinyume na mapenzi yake.

Kimani akionyesha kushukuru, alieleza haya yote kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba hatimaye yupo nyumbani kwao eneo la Mutang'a.

"Asanteni nyote kwa maombi na kunijali kwenu, mama yangu alikuja kunitoa Mathare. Sasa ninaishi naye nyumbani kwake Murang'a huku nikijaribu kuyarejesha maisha yangu," Mbugua aliandika

Haya yanajili baada ya mwanahabari huyu kutoa wito kupitia ukurasa wake wa Twitter akiomba wanamitandao kuwasinikiza wazazi wake kumtoa katika hospitali hiyo ya kiakili.

Kimani aliendelea kudokeza kwamba wazazi walikuwa wamemwachilia kutokana na matatizo ya kiakili ambayo yalisababishwa na matumizi ya dawa za kulevya.

"Natoa wito kwa wote wanaonifahamu kuwaomba wazazi wangu waniruhusu nitoke katika hospitali ya Mathare. Nilikuja hapa baada ya kipindi kifupi cha kiakili tarehe 4 Agosti na kuruhusiwa tarehe 10 mwezi huo huo. Wazazi wangu wameondoka na kuniacha hapa ili kuniadhibu,” Kimani alitweet.

Mamake alikana madai hayo na kusema hawakumtenga kama anavyodai, Ila baada ya uchunguzi kufanywa na madaktari walionelea ingekuwa bora zaidi iwapo angekaa kwenye kituo hicho chini ya uangalizi wa wauguzi.

Mamake Mbugua aliwafafanua kwamba mwanawe alikuwa kwenye kipindi cha mwisho cha matibabu hivyo hangeruhusiwa kabla hajakamilisha kipindi hicho.