Fahamu baadhi ya Wakenya maarufu walioandika vitabu vya simulizi za maisha yao

Lupita Nyong'o anaongoza orodha hiyo ambapo mswada wake wa Sulwe umeshabikiwa kwa jinsi alivyoutunga.

Muhtasari

• Waandishi hao wengi ni wasanii katika vitivo mbalimbali vya sanaa na amabo walionesha weledi wao katika kutunga hadithi kupitia vitabu.

Baadhi ya watu maarufu nchini walioandika vitabu
Baadhi ya watu maarufu nchini walioandika vitabu
Image: Maktaba

Njia pekee ya kujieleza tena kwa mapana na marefu ni kupitia simulizi za maandishi. Nchini Kenya, wapo wasanii wengi ambao wamejinafasi vizuri katika kuelezea matukio si tu kupitia video bali pia katika uandishi wa miswada mbalimbali.

Wengi wanaweza sema kuwa wasanii haswa waigizaji wa filamu na wanamuziki wana weledi mkubwa katika kutunga na kusimulia matukio na hadithi, lakini ifahamike kuwa simulizi katika filamu na nyimbo ni tofauti kidogo na simulizi katika miswada ya riwaya na hadithi fupi.

Katika Makala haya, Radiojambo.co.ke inakuandalia baadhi ya watu maarufu katika Sanaa ambao wamechukua hatua hata zaidi na kuandika miswada ambayo inaelezea hadithi za kusisimua.

Fancy Fingers

Msanii maarufu kutoka kundi la Sauti Sol ambaye jina halisi ni Polycarp Otieno. Mwishoni mwa mwaka jana alidokeza kupitia ukurasa wake wa Twitter kuhusu kuachia kitabu chake chenye maudhui ya watoto chenye mada ‘Written in the Stars’

Fancy Fingers
Fancy Fingers
Image: hisani

Katika kitabu hicho ambacho simulizi kubwa ni kuhusu baba anayesimulia hadithi kwa mtoto wake, Fancy alieleza kwamba msukumo mkubwa ni kutokana na simulizi za kiafrika ambazo zinaendana na watoto wa Kiafrika.

“Vitabu vya Kiafrika vinavyohusiana na watoto wa Kiafrika katika mazingira ya Kiafrika. Ninawasilisha kwako, "WRITTEN IN THE STARS". Ya kwanza kati ya nyingi kuja chini ya mfululizo wa "Papa na mimi"” Fancy Fingers aliandika.

Kitabu hiki kiliasisiwa na Polycarp 'Fancy Fingers' kikaandikwa na Melissa Wakhu na kuonyeshwa na Mathew Odwyre, mwigizaji wa michoro.

Lupita Nyong’o

Mwigizaji maarufu katika filamu za Hollywood ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar mwaka 2014. Hata ingawa anaishi sana ughaibuni lakini ni Mkenya – mtoto wa gavana wa Kisumu Profesa Anyang Nyong’o.

Lupita wiki iliyopita alikuwa anasherehekea miaka 3 tangu kuchapishwa kwa mswada wake wa kwanza kwa jina Sulwe.

Lupita Nyong'o
Lupita Nyong'o

Kama tu kitabu cha Fancy Fingers, kitabu cha Lupita pia kina maudhui yanayowalenga watoto wadogo. Katika simulizi hiyo, msichana kwa jina Sulwe ambaye ni mweusi kupindukia anaonekana kuichukia rangi ya ngozi yake na kutaka kupata uwezo wa kuibadilisha ili kuwa kama wazungu.

Nyong’o aliandika kitabu hicho kuwausia watoto wa Kiafrika kujikubali jinsi walivyo kwani uzuri na urembo hutokana ndani na wala si muonekano wa rangi ya ngozi.

Terence Creative

Mwigizaji wa humu nchini ambaye alipata umaarufu zaidi mwaka jana kutokana na filamu zake za Wash Wash akiigiza kama mwanaume tajiri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

terance creative
terance creative

Terence katika maahojiano yake ya awali, aliwahi kudokeza kwamba alikulia maisha yenye ugumu mno katika mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi ambapo alikuwa akiishi na nyanya yake. Nyanya yake alikuwa ni mgemaji wa mvinyo haramu na baadae alijipata katika hifadhi ya kuwalea watoto wasiokuwa na wazazi.

Akipakia picha hiyo akiwa na kitabu chake chenye mada ‘Hope About’ alisema kwamba katika maisha hakuna kitu amabcho hajakipitia katika mkondo wa kujaribu kutoboa tundu la maisha.

Janet Mbugua

Aliyekuwa mtangazaji wa runinga aliandika kitabu chake kinachosimulia masuala ya mtoto wa kike chenye mada ‘My First Time’, kitabu ambacho kinalenga kupinga unyanyapaa wa hedhi, kuongeza ufahamu juu ya ushirikishwaji wa hedhi na kutoa hoja kwa Haki ya Hedhi, kupitia hadithi mbalimbali na tofauti za akaunti za kwanza zilizoangaziwa katika chapisho.

Image: jant mbugua

Dada Janet Mbugua aliacha kazi yake ya uanahabari miaka michache iliyopita, amejitolea maisha yake katika kutetea mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla katika jamii ya Kenya.

Watu maarufu wengine amabo pia wametunga miswada ni mwanahabari marufu Jeff Koinange ambaye ameelezea hadithi yake katika kitabu chake cha ‘Through my African Eye’, mwanaharakati Boniface Mwangi kupitia kitabu chake cha ‘Unbounded’ miongoni mwa wengine wengi.