Davido aghairi tamasha la Marekani kufuatia kifo cha mwanawe

Tamasha hilo lilipangwa kufanyika Novemba 18 katika uwanja wa State Farm Arena jijini Atlanta, Georgia.

Muhtasari

•Davido bado hajasema lolote kuhusu kifo cha mwanawe Ifeanyi Adeleke ingawa ameondoa machapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu tamasha hilo.

Image: INSTAGRAM// DAVIDO

Mwimbaji mashuhuri wa Nigeria Davido huenda asifanye tamasha lake la Amerika la ‘AWAY’ ambalo lilikuwa limesubiriwa kwa hamu kufuatia kifo cha mtoto wake na mpenziwe Chioma.

Davido bado hajasema lolote kuhusu kifo cha mwanawe Ifeanyi Adeleke ingawa ameondoa machapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu tamasha hilo.

Tamasha hilo lilipangwa kufanyika Novemba 18 katika uwanja wa State Farm Arena jijini Atlanta, Georgia.

Tamasha hilo lilikusudiwa kuwashirikisha Kizz Daniel, Wande Coal, Lojay, Pheelz, Oxlade, Buju, Focalistc na Victony.

Davido pia alitarajiwa kufanya kazi kwenye mradi na kampuni ya Puma wiki hii, lakini kampuni hiyo imeahirisha.

Mtoto wa Davido, Ifeanyi Adeleke alikufa maji katika kidimbwi cha kuogelea nyumbani kwake nchini Nigeria.

Ripoti zinaonyesha kuwa Ifeanyi alikuwa ameachwa chini ya uangalizi wa yaya wake wakati ajali hiyo ilipotokea.

Wakati huo, Davido na Chioma walikuwa wamesafiri kwenda jimbo lingine na kumwacha mtoto wao.