Natafuta katoto ka Kimasai,'Stevo Simple Boy asema huku akifichua sababu ya kuenda Loitoktok

Kulingana na video hiyo, Stevo anasikika akisema kwamba alikuwa akisafiri kwenda Loitoktok.

Muhtasari
  • Naam, mbali na muziki, Stevo pia anajulikana kwa misemo yake ya kipekee ikiwa ni pamoja na "Freshi barida" kati ya mingine mingi
Msanii Stevo Simple amezungumzia kwa hisia kali himizo la wimbo wake mpya
Msanii Stevo Simple amezungumzia kwa hisia kali himizo la wimbo wake mpya
Image: instagram

Stevo Simple Boy ni mmoja wa wasanii bora nchini Kenya waliojizolea umaarufu baada ya kuachia wimbo wa Mihadarati.

Naam, mbali na muziki, Stevo pia anajulikana kwa misemo yake ya kipekee ikiwa ni pamoja na "Freshi barida" kati ya mingine mingi.

Stevo Simple Boy alishiriki video kwenye hadithi zake za Instagram. Kulingana na video hiyo, Stevo anasikika akisema kwamba alikuwa akisafiri kwenda Loitoktok.

Kwake, madhumuni ya kwenda Loitoktok ni kutafuta msichana mzuri wa Kimasai wa kuoa.

"Naenda Loitoktok kuchukua binti wa kimaasai awe mke wangu ausio. Ndio manake" alisema.

Stevo Simple Boy anaweza kuwa amepata upendo wa maisha yake tena, kulingana na hisia zake

Msanii huyo amekuwa akivuma sana baada ya kuwa kwenye mapenzi na wanwake tofauti, huku wakiachana muda usio kuwa mrefu.