Ulijaza nafasi iliyokuwa moyoni mwangu-Diana Marua amwandikia mwanawe ujumbe mtamu

Yeye ni mama mwenye upendo wa watoto wanne Morgan Bahati Heaven Bahati, Majesty Bahati na Malaika Bahati.

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Diana ameshiriki video ya kupendeza ya bintiye Malaika na yeye walipokuwa wakiota jua nje ya nyumba yao 
Diana Marua

Diana Marua amekuwa mama bora kwa watoto wake kila wakati . Kuanzia video anazoshiriki kwenye mitandao ya kijamii hadi kwenye chapisho analotoa na kutoa maoni ni dhahiri kwamba yeye ni mama anayejali.

Yeye ni mama mwenye upendo wa watoto wanne Morgan Bahati Heaven Bahati, Majesty Bahati na Malaika Bahati.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Diana ameshiriki video ya kupendeza ya bintiye Malaika na yeye walipokuwa wakiota jua nje ya nyumba yao .

Video hiyo imevutia mastaa wenzake na kuvutia maoni kutoka kwa mashabiki wake, huku wakimlimbikizia sifa Diana kwa malezi yake Kwenye video hiyo Diana ameelezea mapenzi yake kwa bintiye huku akisema kuwa alikuja katika maisha yake na kujaza nafasi ambayo hakujua ipo.

Ulikuja maishani mwangu na kujaza nafasi tupu moyoni mwangu ambayo sikujua iko+. I love you Daddy’s girl @malaika_bahati ❤️,"Aliandika Diana.