Diamond amnunulia mpenziwe Zuchu mkufu wa Ksh 5M

Mwezi mmoja uliopita Zuchu naye alimnunulia Diamond cheni kama hiyo kwa Ksh 29.

Muhtasari

• Wawili hao kwa zaidi ya mwaka mmoja wamekuwa wakioneshana mapenzi yao mitandaoni huku baadhi wakihisi ni kiki.

Diamond amnunulia Zuchu cheni kali
Diamond amnunulia Zuchu cheni kali
Image: Instagram

Msanii namba moja wa muda wote ukanda wa Afrika Mashariki Diamond Platnumz kwa mara nyingine amedhihirisha upendo wake kwa mpenzi wake Zuchu kwa kumnunulia cheni ya thamani shilingi milioni 94 za Kitanzania sawa na milioni 5 za Kenya.

Msanii huyo alionesha zawadi hiyo kwenye instastory yake ambapo ilikuwa tayari imekaa penyewe – kwa maana kwamba tayari Zuchu alikuwa amevishwa shingoni. Cheni hiyo ilikuwa imeandikwa jina la Zuchu.

Wiki chache zilizopita, Diamond aliweka wazi kuwa Zuchu ni mpenzi wake huku akimsherehekea kuzaliwa kwake.

Diamond japo alipokea masimango mengi kutoka kwa baadhi ya watu waliomsuta kwa kumtaja Zuchu kama mkewe hali ya kuwa bado hajamfungisha ndoa wala kumvisha pete, alisisitiza kuwa hapo ndipo moyo wake wa mapenzi umetuana na kutabahari pasi na shruti yoyote.

Itakumbukwa mwezi mmoja uliopita Zuchu naye alimnunulia Diamond cheni ya thamani ghali na kumvisha kabla ya kumbusu hadharani.

Kulingana na runinga ya Wasafi, Zuchu aligharimika kwa kuzama mfukoni na kuibuka na kima cha shilingi milioni 29 za Tanzania na pia kuchukua muda wa miezi miwili kimya kimya kufanikisha zawadi hii ya kustukiza ambayo alimkabidhi bosi wake kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa aliyoiadhimisha wiki mbili zilizopita.

Diamond kipindi hicho alimshukuru Zuchu pakubwa huku akimtaja kama mtu anayejua kile anachokihitaji na wala hajawahi kosea katika zawadi zake kwake.

“Maneno hayawezi elezea shukrani yangu kwa hili Zuuh, nisije nitateleza kuandika waandishi wakapata stori. Ila jua nakushukuru sana na siku zote utaendelea kuwa pale,” Diamond alimshukuru.

Inasubiriwa Zuchu atatamka nini kuhusu Zawadi hiyo kutoka kwa mpenzi wake Simba.