Diamond ambusu Zuchu hadharani baada ya kupokea zawadi yake ya cheni ya dhahabu

Zuchu alitumia kiasi cha milioni 29 kumwandalia Diamond zawadi hiyo ya dhahabu.

Muhtasari

• “Ishi sana tajiri, huna baya. Siku zote utakuwa shujaa wangu” Zuchu aliandika.

• Diamond alionekana kuweka maneno yake kwenye mizani alipokuwa akimshukuru Zuchu kwa zawadi hiyo.

Zuchu amkabidhi Diamond zawadi ya cheni ya dhahabu
Zuchu amkabidhi Diamond zawadi ya cheni ya dhahabu
Image: screengrab

Malkia wa muziki kutoka lebo ya WCB Wasafi, Zuchu amemfanyia bosi wake Diamond Platnumz jambo la kustukiza kwa zawadi ghali mno.

Zuchu alimnunulia Diamond zawadi ya cheni ghali iliyoundwa kutoka kwa madini ya dhahabu ambayo iliundwa kwa njia mahususi kwa ajili ya msanii huyo nambari moja wa muda wote katika ukanda wa Afrika mashariki.

Cheni hiyo ilitengenezwa na jamaa mmoja kwa jina Dr Smile kupitia biashara yake ya Shohreh Custom Made.

Katika video hiyo ambayo Diamond alipakia kwenye Instagram, alimshukuru Zuchu kwa zawadi hiyo ambayo hakuwa anaitarajia kabisa na kusema kweli amehisi upendo na kujaliwa.

Vile vile msanii huyo katika shukrani yake alionekana kuwa mtu mwenye tahadhari kubwa kwa kutilia kwenye mizani maneno yake ili kutowapa faida wanoko na wadaku ambao muda wote wamekuwa wakikisia wasanii hao wawili wapo katika mahusiano ya kimapenzi.

“Maneno hayawezi elezea shukrani yangu kwa hili Zuuh, nisije nitateleza kuandika waandishi wakapata stori. Ila jua nakushukuru sana na siku zote utaendelea kuwa pale,” Diamond alimshukuru.

Zuchu naye hakuwa mchache wa kuonesha fadhila zake si tu kwa vitendo bali kwa maneno kwani alimshukuru sana Diamond kwa kumfanya kuwa jina kubwa ambalo sasa hivi ni gumzo katika janibu zote kutokana na muziki wake amabo umepenya kila kichochoro.

“Ishi sana tajiri, huna baya. Siku zote utakuwa shujaa wangu” Zuchu aliandika.

Kulingana na runinga ya Wasafi, Zuchu aligharimika kwa kuzama mfukoni na kuibuka na kima cha shilingi milioni 29 za Tanzania na pia kuchukua muda wa miezi miwili kimya kimya kufanikisha zawadi hii ya kustukiza ambayo alimkabidhi bosi wake kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa aliyoiadhimisha wiki mbili zilizopita.