Namshauri Zuchu kuwekeza mtoto kwa Diamond kama anataka mali yake - Baba Levo

Mpaka sasa Diamond ana nyumba mbili South Afrika na pia amenunua viwanja hekari 3 Mikocheni - Baba Levo.

Muhtasari

• Anachokifanya Diamond ni kuwekeza mali kwa ajili ya watoto wake na ndio maana nilimshauri Zuchu kuingia kwenye mirathi kwa kumzalia - Baba Levo.

Baba Levo amshauri Zuchu kumzalia Diamond Platnumz ili kuingia kwenye mirathi yake
Baba Levo amshauri Zuchu kumzalia Diamond Platnumz ili kuingia kwenye mirathi yake
Image: Instagram

Kama ilivyo kawaida, baada ya picha kuibuka mitandaoni ikionesha jumba ambalo lilisemekana kumilikiwa na msanii Diamond Platnumz nchini Afrika Kusini, chawa wake Baba Levo amezungumza.

Itakumbukwa wiki jana picha hizo zilisambazwa watu wakisema kuwa Diamond amenunua mjumba wa kifahari karibu tu na makaazi ya familia yake ya awali, watoto wake na aliyekuwa mkewe Zari Hassan.

Kando na hayo, pia ilisemekana kuwa msanii huyo nambari moja kwa muda wote ukanda wa Afrika mashariki amenunua kiwanja katika mtaa wa kifahari wa Mikocheni, viungani mwa jiji la Dar es Salaam.

Baba Levo akizungumzia hili na wanablogu aliweka wazi kuwa si kiwanja kimoja bali ni viwanja vitatu na kiwanja kimoja katika eneo hilo la Mikocheni kinauzwa kwa takribani bilioni moja pesa za Tanzania bara.

“Hekari tatu Mikocheni si mchezo, kila hekari ni bilioni. Kwa hiyo nip loti katika ufukwe na ni moja kati ya mali ambayo Diamond anazidi kuwekeza katika mazingira yake. Hamna msanii amabye anaweza kumweza Diamond kwa hela hapa Afrika Mashariki, hakuna,” Baba Levo alisema.

Aliweka wazi kuwa msanii huyo bosi wa Wasafi mpaka sasa amenunua nyumba mbili Afrika Kusini na kumtania msanii Zuchu ambaye amekuwa akisemekana kuwa mpenzi wake kuwa alimshauri azae mtoto ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuingia katika orodha ya mirathi ya mali ya Diamond ambayo anazidi kuiwekeza katika kila kona ya dunia.

“Mpaka sasa Diamond ana nyumba mbili Afrika Kusini, na anachokifanya ni kuongezea watoto wake mali, ndio maana nilikuwa namwambia Zuchu ni bora ungezaa haraka ukimbizane na hizi mali. Maanake huwezi kukimbizana na mali ya mtu na huna chochote ulichowekeza kwake. Wekeza mtoto ukimbizane na mali,” Baba Levo alimshauri Zuchu.

Kwa muda mrefu Zuchu amekuwa akisemekana kutoka kimapenzi na bos wake Diamond Platnumz mpaka machawa wa lebo hiyo wamekuwa wakieneza habari kama hizo ila bado wahusika wakuu ambao ni wasanii hao wawili hakuna aliyefunguka ukweli unaozunguka suala hilo.