Mwijaku asema hana urafiki na H-Baba, Baba Levo, "Wasafi Bet tuko pamoja sababu ya kazi tu"

Mwijaku alisema wawili hao ni machawa wa chini ambao hata elimu ya darasa la saba hawana kulinganishwa na yeye mwenye digrii mbili.

Muhtasari

• “Nimewashinda elimu, nimewashinda maisha nimewashinda upeo, nimewashinda kila kitu." - Mwijaku.

Mwijaku awasuta vikali Baba Levo na H Baba
Mwijaku awasuta vikali Baba Levo na H Baba
Image: instagram

Mtangazaji wa Clouds, Mwijaku amewajibu vikali watu wanaomliganisha na machawa wengine wa Diamond Platnumz kama Baba Levo na H Baba.

Mwijaku ambaye ni mtu mwenye utata sana haswa kwa uhusiano wake na Diamond. Licha ya kumsuta vikali na kuonekana kuwatetea Harmonize na Alikiba, bado mtangazaji huyo ni mmoja wa mabalozi wa biashara ya jukwaa la ubashiri la Wasafi Bet ambalo ni la Diamond Platnumz.

Mabalozi wenzake ni pamoja na machawa Baba Levo na msanii mkongwe H Baba. Alipoulizwa uhusiano wake na wale wawili, Mwijaku alisema kwamba anafuata Wasafi kwa faida za kibiashara tu.

Pia aliwataka watu kukoma kumlinganisha na Baba Levo na H Baba kwa kile alisema kwamba hawala kutoka sahani moja na hawako kiwango sawa kabisa na wawili hao.

Alitolea mfano akasema kwamba yeye ana akili zilizopitiliza na amabzo zimeboreshwa na elimu aliyoipata kutoka vyuo viwili maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki kulinganishwa na hao wawili aliosema hawana elimu hata kidogo.

“Sina urafiki na Baba Levo wala H Baba. Ile ni kazi, sina urafiki na watu wasiokuwa na akili. Unaniweka vipi pamoja na watu ambao hawana elimu. Mimi nina IQ ya kiwango cha juu, nina digrii mbili kutoka vyuo vinavyotambulika duniani. Unaniweka vipi na watu ambao hata darasa lac saba hawajui,” Mwijaku alisema katika mahojiano na mwanablogu.

Alizidi kuwakebehi kwa kusema kwamba H Baba na Baba Levo ni watu amewashinda katika kila kitu na hata anaishi na mkewe katika maisha mazuri kuwaliko wawili hao.

“Nimewashinda elimu, nimewashinda maisha nimewashinda upeo, nimewashinda kila kitu. Mimi ndio kijana pekee ambaye ninaishi na mke wangu na ambaye tunaishi maisha ya kiwango sawa,” Mwijaku alisema.