Kanye West asherehekea kuzaliwa kwa mwanawe nyumbani kwa Kim Kardashian

ni wiki jana tu ambapo talaka yao ilikamilishwa mahakamani, Kanye atakuwa analipa Ksh 24M kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya wanawe.

Muhtasari

• Haijulikani kama wanafamilia wengine wa Kim walikuwepo kwenye tafrija hiyo.

kanye West na familia yake.
kanye West na familia yake.
Image: BBC News

Blogu ya TMZ nchini Marekani imeripoti kuwa msanii maarufu wa rap Kanye West na aliyekuwa mkewe, Kim Kardashian walikutana kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa mchakato wa talaka yao.

Inaripotiwa kuwa Kanye West ndiye aliyeenda kwenye jumba la kifahari ambalo Kim Kardashian anaishi pamoja na wamawe.

Wawili hao walikutana kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe wa kiume aliyekuwa akifikisha miaka 7.

Chapisho hilo linaripoti kwamba haikujulikana mara moja ikiwa wanafamilia wengine wa Kim pia walihudhuria sherehe hiyo.

“Ye alitumia saa kadhaa katika eneo la Kim's Hidden Hills Jumatatu usiku kwa siku ya kuzaliwa ya Saint. Haijulikani kama wanafamilia wengine wa Kim walikuwepo kwenye tafrija hiyo, lakini kuhudhuria kwa Kanye kunazungumza kweli kuhusu dhamira ya Kim ya kumweka Kanye katika maisha ya watoto wao ... bila kujali anapitia nini hadharani,” TMZ walisema.

Mapema wiki jana, Kim na Kanye walisuluhisha talaka yao, ambapo atakuwa anatengana na kima cha $200,000 sawa na shilingi za Kenya milioni 24 kwa mwezi kama matunzo ya mtoto na ilikubaliwa watakuwa na "ufikiaji sawa" kwa watoto.

Kim na Kanye ndoa yao ya miaka 12 iliingia doa mapema mwaka huu baada ya mwanamitindo huyo ambaye pia anajiongeza kama mzalishaji wa maudhui ya kihalisia kwenye runinga kumtuhumu mwanamuziki Kanye kwa kumnyima uhuru katika ndoa yao.