Miaka 28 ya ndoa: Rev Kathy Kiuna ambusu mumewe mbele ya kanisa, "Nakulombotove"

Wanandoa hao pia ni waanzilishi wa kanisa la Jubille Christian Church, JCC, na walikuwa wakisherehekea miaka 28 ya ndoa yao.

Muhtasari

• Kathy Kiuna hakuaibika kulipanda busu la ajabu midomoni mwa mumewe mchungaji Allan Kiuna huku waumini wakishuhudia.

Walokole, Kathy na Allan Kiuna wakilana denda kanisani
Walokole, Kathy na Allan Kiuna wakilana denda kanisani
Image: Instagram

Mchungaji Kathy Kiuna wikendi iliyopita alidhihirisha upendo wake wa miaka mingi kwa mume wake ambaye pia ni mchungaji mwenza Allan Kiuna hadharani mbele ya madhabahu macho kadhaa ya waumini yakiwashuhudia.

Kathy alimkaribia mumewe na kulipanda bonge la busu mdomoni mwake huku akimwachia ujumbe maridhawa kuwa tangu mwanzo alimpenda yeye na mpaka siku ya mwisho bado upendo wake utabaki kumjua yeye tu.

“Ni kumbukumbu ya miaka yetu na upendo wa maisha yangu. Ni vibe gani ya kufanya maisha na rafiki yangu bora. Tunapendana zaidi kuliko tulipoanza. Inaweza tu kuwa Mungu. Utukufu uwe kwa Mungu. @bishopkiuna nakulombotove,” Reverand Kathy Kiuna alisema.

Wanandoa wa kidini na waanzilishi wa Jubilee Christian Church (JCC) walikuwa wanasherehekea miaka 28 ya ndoa kwa heshima kubwa.

“Ni njia nzuri jinsi gani ya Kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa ndoa yetu na kumbukumbu ya mwaka wangu @bishopkiuna, karibu miongo 3 ya kufanya maisha pamoja. Mungu amekuwa mwema sana kwetu na tunashukuru 🙏. Tulikuja, tukala, tukacheza,” aliandika kwenye video moja.

Waumini wao walifurahia jinsi familia hiyo ya walokole wanaoneshana upendo bila kuogopa na kuwasherehekea kwa jumbe nzuri.

“Kumbukumbu nzuri sana, tunawapenda pakubwa,” mwimbaji wa injili Kambua aliandika.

“Asante kwa kuifanya ndoa ionekane nzuri na ya kupendeza. Asante kwa kutuonyesha kuwa inafanya kazi kweli. Asante kwa kuwa mifano mizuri...” Monica Nyambz aliandika.