Wahu afunguka alitaka kutoroka Nameless baada ya miaka 2 ya ndoa

Wahu alisema ilibidi wameendea ushauri ili kuimarisha ndoa yao.

Muhtasari

• Alisema kipindi hicho alikwa anakasirika sana lakini sasa amezoea na maisha yanaenda vizuri.

Wahu
Wahu
Image: Instagram

Msanii Wahu amefunguka kuwa ndoa si kitu cha kukata tamaa hivyo haraka kwani ni hatua ambazo kama wawili wapendanao hawatakuwa na subiria basi itawashinda.

Akizungumzia ufanisi mkubwa wa ndoa yake na mumewe, mwanamuziki Nameless, Wahu alisema kuwa miaka ya mwanzoni hawakuwa wanaelewana kabisa na alitaka kuondokea ndoa hiyo baada ya miaka 2 tu.

Wahu alikuwa anazungumza na mkewe mchekeshaji Njugush, Celestine Ndinda ambapo alifunguka kuwa muda mwingi katika miaka ya awali alikuwa anatoroka nyumbani baada ya kukosana na Nameless kwa kitu kidogo tu – mpaka wakati mmoja aliondoka na kwenda kutafuta nyumba yake binafsi.

Lakini je, ni vipi alianza kuzoea na kuamua kuacha tabia ya kutoroka?

Wahu alisema kuwa ilifika mahali akakomaa kiakili na kujiaminisha kuwa kutoroka suluhu si kulisuluhisha.

“Inafika mahali unasema wewe ndio uko rafiki yangu, na mimi ndio niko, wacha tung'ang'ane. Itabidi sasa tupendane. Lakini bila shaka hapo mwanzoni, weeh! Kwanza ile miaka miwili ya awali, nilikuwa nishaenda hata kutafuta nyumba, Nilikuwa najiambia kuwa mimi siwezi kosa kitu chochote hii Nairobi kwa sababu najitegemea,” Wahu alisema.

Kando na kukomaa, alisema kuwa anadhani kufikiria kwake sasa na kipindi kile ni nyakati mbili zilizotofautiana huku akisema kukasirika kwake kumepungua, jambo ambalo limerahisisha maisha yake na mumewe.

“Tofauti ni, sasa mimi nimeacha kukasirika sana. Viatu bado vinaachwa mahali vinaachwa Nimezoea. Nimesema, hata mabadiliko. Tuelienda ushauri tukaambiwa watu hubadilika mara chache. Unachagua kile kitakachokusisitiza na kile kitakachokufurahisha,” Wahu alishauri.

Wawili hao wamedumu pamoja kwa miaka 25 sasa, miaka 17 ikiwa ni ndoa rasmi waliyofunga mwaka 2004.

Mwezi Septemba wakati wa kusherehekea kufikisha miaka 17 ya ndoa, Wahu alidokeza kuwa kuwa blogu fulani maarufu nchini kipindi hicho iliyotabiri kuwa ndoa yao haingemaliza hata miaka 2.