“Tafuta msichana mrembo kama mimi” – Zari kwa mwanawe baada ya kufikisha miaka 18

"Ni furaha yangu, wewe nenda kutana na wasichana, ni jambo zuri, nalipenda kwenye wanangu, lakini hakikisha hao wasichana ni warembo kama mimi, watakua kama mimi, wenye akili kama mimi na wachapakazi kama mimi mama yenu."

Muhtasari

• Mama yake alimshauri kwamba si vibaya kuwa na mpenzi, haswa baada ya kufikisha miaka 18 kwenda mbele lakini akamuasa kufanya chaguo la maana.

Zari na mwanawe
Zari na mwanawe
Image: Instagram

Zari ni mama mwenye furaha baada ya mwanawe mwingine kufikisha umri wa kuwa mtu mzima, miaka 18.

Kupitia Instagram yake, Zari alipakia video akimpakulia vipande vya ushauri kijana huyo kwa jina LilQ na kumkaribisha rasmi kwenye chama cha watu wazima wa kujifanyia maamuzi wenyewe.

Katika ushauri huo, kijana huyo alionekana kuaibika kuzungumza na mama yake haswa suala la kimapenzi mpaka pale mwenzake akathibitisha kwamba ana mpenzi.

Mama yake alimshauri kwamba si vibaya kuwa na mpenzi, haswa baada ya kufikisha miaka 18 kwenda mbele lakini akamuasa kufanya chaguo la maana.

Zari alimtaka mwanawe kutafuta msichana mrembo, mchapakazi na mwenye akili kama yeye mama yake.

“Mnajua hiki kizazi kimeharibika, hata hivyo mimi sina tatizo kuwaona mkitoka na wasichana. Ni furaha yangu, wewe nenda kutana na wasichana, ni jambo zuri, nalipenda kwenye wanangu, lakini hakikisha hao wasichana ni warembo kama mimi, watakua kama mimi, wenye akili kama mimi na wachapakazi kama mimi mama yenu,” Zari alishauri wanawe.

Lilq Qunicy ni mtoto wa tatu wa Zari aliyezaa na marehemu mumewe Ivan Don Seemwanga kabla ya kuolewa tena na Diamond Platnumz na kuzaa watoto wengine wawili, Tiffah na Nillan.