Pete Davidson afuta tattoo ya Kim Kardashian miezi 5 tu baada ya kuachana

Davidson na Kardashian walianzisha uhusiano wao miezi michache tu baada ya mwanamitindo huyo kuvunja ndoa yake na Kanye West.

Muhtasari

• Mchekeshaji huyo alikuwa amechora tattoo ya Kardashian na wanawe katika kifua chake lakini baada ya kuachana, alionekana bila hizo tattoo.

Pete afuta tattoo ya Kardashian
Pete afuta tattoo ya Kardashian
Image: Page Six

Pete Davidson, ambaye ni mpenzi wa hivi karibuni wa mmwanamitindo Kim Kardashian ameripotiwa kufuta mchoro wa tattoo wa mwanamitindo huyo aliouchora kama njia ya kuonesha mapenzi yake kwake.

Kulingana na jarida la Page Six, mchekeshaji Pete Davidson ambaye waliachana na Kardashian takribani miezi mitano iliyopita alionekana kwa mara ya kwanza bila shati na hapo ndipo mapaparazzi walibaini kuwa tattoo ya jina la Kim haipo tena kifuani mwake.

“Pete Davidson alienda bila shati alipokuwa akifurahia safari ya kwenda Hawaii na mpenzi wake aliyedaiwa kuwa ni Chase Sui Wonders mwishoni mwa juma - na kando na kuonyesha kifua chake baharini, mcheshi huyo pia alifichua tattoo zake zilizowekwa kwa ajili ya Kim Kardashian zilionekana kutoweka,” Jarida hilo liliripoti.

Nyota huyo wa "Meet Cute" mwenye umri wa miaka 29, aliweka tattoo mwilini mwake kwa ajili ya kumuenzi mpenzi wake wa wakati huo, akichora tatoo kadhaa ambazo zilimrejelea Kardashian na hata watoto wake - lakini wino huo haukuonekana wakati wa kujivinjari kwake baharini.

Davidson aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Kim miezi michache tu baada ya mwanamitindo huyo kuiasi ndoa yake na rapa Kanye West – ndoa ambayo ilisemekana kuwa ya miaka 12.

Baadae alielekea mahakamani kutaka talaka rasmi, jambo ambalo Kanye alikuwa akilipinga vikali na hakuwa anataka familia yake kutenganishwa naye.

Hata hivyo kesi hiyo ilikamilika mwishoni mwa mwaka jana ambapo msanii huyo alitakiwa kutoa zaidi ya milioni 24 pesa za Kenya kila mwezi kama hela za matunzo na malezi ya watoto wake na Kim Kardashian.