Trio Mio: Siwezi oga maji baridi!

Msanii huyo alisema kuwa akiwa shule alikuwa anaoga maji baridi lakini tangu kumaliza shule, suala hilo hawezi kulivumilia.

Muhtasari

• Trio Mio alikamilisha masomo yake ya sekondari mwishoni mwa mwaka jana.

Trio Mio
Trio Mio
Image: Instagram

Trio Mio, rapa mchanga Zaidi kuwahi kutokea nchini ambaye alimaliza shule mwishoni mwa mwaka jana amezungumza kile ambacho anakikosa katika maisha yake nje ya shule.

Trio Mio alifikisha miaka 18 mwaka jana, mieizi michache akisubiria kuukalia mtihani wake wa KCSE.

Kwa kawaida, watu wengi haswa wanafunzi huwa hawataki kuzungumzia kitu chochote kizuri kutoka maisha yao ya shuleni, jambo ambalo wanasema ni kama jela bila uhuru wa kufanya mambo yao. Lakini kwa Trio Mio, hali ni tofauti kwani kuna mambo mengi ameyakosa ambayo alikuwa anafurahia akiwa shuleni.

Alisema kuwa nyumbani huwa anakoga kwa maji moto lakini kama kuna kitu kikubwa anachokikosa Zaidi enzi za shuleni ni kukoga maji baridi.

“Kama kuna kitu nakosa Zaidi ni maji baridi. Siku hizi ninakoga maji moto nyumbani, namkosa mwalimu wetu mkuu, marafiki zangu na kushiriki katika burudani ya shuleni,” Trio Mio alisema.

Msanii huyo pia alifutilia mbali uwezekano wa kuendelea na masomo yake baada ya kukamiisha kidato cha nne mwishoni mwa mwaka jana.

Alisema lengo lake kuu ni kuwaunganisha vijana wenzake kupata ajira za kuwalipia bili za maishani, akidokeza tayari ameingia kwenye mtakaba wa ushirikiano na kampuni moja ya kusambaza pipi ambapo anataka vijana wajiunge ili kupewa kandarasi ya kuzunguza pipi na kupata kuzindikiza mkono kinywani.