Diana na Bahati waramba dili nono la kuwa mabalozi wa utalii wa Dubai

Bahati na mkewe Diana walionekana walizuru maeneo mbali mbali yenye hadhi ya nyota tano.

Muhtasari

• Bahati na mkewe waliondoka nchini siku mbili zilizopita kwenda ziara ya kujivinjari nje ya nchi.

• Wapenzi hao wamekuwa wakipakia kila tukio la ziara hiyo yao kwenye kurasa zao za Instagram na YouTube,

Diana na Bahati wakula dili la ubalozi Dubai
Diana na Bahati wakula dili la ubalozi Dubai
Image: Instastory

Bahati Kioko na mkewe Diana Marua ni familia yenye tabasamu zisizoisha. Hii ni baada ya wawili hao kuramba dili nono la kuteuliwa kama mabalozi wa kuutangaza utalii wa Dubai, wakiwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Wawili hao waliondoka nchini kenya siku mbili zilizopita wakisema kwamba walikuwa wanaenda ziara ya kula bata na kujivinjari nje ya nchi.

Hata hivyo, hawakuweka wazi ni nchi gani walikuwa wanakwenda kubarizi lakini siku ya Jumatano kupitia kurasa zao za mtandao wa Instagram, waliweka wazi kwamba wako katika taifa la Miliki za Kiarabu katika jiji la Dubai.

Ziara yao kwenda kule sasa imebainika kwamba haikuwa ziara ya kwenda kubarizi tu bali kwa namna fulanio inaweza tajwa kuwa ziara ya kikazi kwani walikwenda kutia saini mkataba wa kuwa mabalozi wa utalii wa Dubai, jiji ambalo ni maarufu duniani kwa ukuaji wa kasi na mandhari ya kupendeza.

Katika tamasha liitwalo Dubai A-Z, wawili hao wakiwa kama mabalozi wa Dubai wakiwakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati watashiriki katika ushindani wa kirafiki na wenzao ambao pia waliteuliwa kuwakilisha ukanda wa Afrika Kusini.

“Ndiooo! Sisi #TheBahati ni Mabalozi Rasmi wa Chapa ya Kenya nchini Dubai na tuko hapa kwa Hisani ya Utalii wa Dubai 😝 Hii ni kukufahamisha tu kuwa tutakuwa kwenye Shindano la kirafiki na Afrika Kusini huku tukikuonyesha #DubaiAtoZ 👊” Diana alidokeza kwenye ukurasa wake wa Instagram.