Vanessa Mdee amuimbia mwanawe wimbo wa injili kwa sauti ya hisia nzito za furaha

“Si kwa majeshi, wala silaha, ni kwa roho mtakatifu. Nguvu za giza zimeshindwa kwa jina la Yesu Kristo…” Vanessa Mdee aliimba.

Muhtasari

• Baadhi ya mashabiki zake walifurahia jinsi anavyomweka Mungu kwanza katika familia yake na Rotimi.

• Wengine walisema kuwa Mdee ni kielelezo tosha kwamba Muda wa Mungu siku zote hauna ubishi.

Vanessa Mdee amuimbia mwanawe kwa hisia nzito za furaha
Vanessa Mdee amuimbia mwanawe kwa hisia nzito za furaha
Image: Instahram

Takribani wiki tatu tangu mwigizaji wa nguvu anayejiongeza pia kama msanii kutoka Marekani Rotimi na mpenzi wake kutoka Tanzania, Vanessa Mdee kuweka wazi kubarikiwa na mtoto wa pili, wanandoa hao wenye furaha wangali kumalzia furaha yao.

Vanessa Mdee mapema Alhamisi asubuhi alipakia video nzuri kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa amempakata mtoto huyo mchanga huku akimuimbia wimbo wa injili kwa sauti yake nzuri iliyosheheni chembechembe za furaha ya mama kwa mwanawe.

“Si kwa majeshi, wala silaha, ni kwa roho mtakatifu. Nguvu za giza zimeshindwa kwa jina la Yesu Kristo…” Vanessa Mdee aliimba akimtazama kwa furaha mtoto wake kwenye mikono yake yenye nguvu za aina yake.

Mashabiki wake ambao muda wote humpa shavu walimhongera kwa kumuita ‘mama wawili’ na kusema kwamba tungo hiyo ya injili aliyokuwa akimuimbia mwanawe ni moja ya nyimbo za kuibua kumbukumbu za mbali sana.

Ubarikiwe Mama wawili, umenikumbusha mbali sana,” Minalisa Tz aliandika.

“Jamani unaonekana vizuri kama yule dada yako mkubwa anayeimba wimbo huo wa injili. Tunakutumia upendo wa hali ya juu kutoka tz ️” Jaques Taste alimpa makopa.

“Hongera sanaaaa kweli wakati wa Mungu ni wakati sahihi,” Next Helen alisema.

“Inashangaza Tu Kiwango cha Uelewa wa Vee Kwenye Maisha️ , MUNGU KWANZA DAIMA + FAMILIA = AMANI” mwingine aligundua.

Familia hiyo katika siku za hivi karibuni wameonekana wakikumbatia Mungu na injili Zaidi ambapo mambo mengi wanayafanya kwenye mitandao yao tofauti, aghalabu humtaja Mungu sana na kumpa sifa kwa kuwakutanisha na kuwajaalia muunganiko wenye furaha na Baraka ya watoto wawili juu chini ya miaka miwili tangu kuweka bayana mahusiano yao.

Siku nne zilizopita, Rotimi pia alipakia video kwenye ukurasa wake akimuimbia kwa furaha mtoto huyo wake ambaye alikuwa amemlaza kwenye kifua chake akiwa amelala chali kwenye kitanda.

“Wakati mwingine Tunapuuza Kushukuru Kwa Mambo Madogo na Rahisi Zaidi ... Nilipokuwa Nimekaa na Mtoto Wangu Kifuani Mwangu na Mwanangu Aliketi na Mama Yake Ilijaza Moyo Wangu na Ilinikumbusha Tu Kuwa Haijalishi Ni Kelele Gani Inatokea Nje Ya Maisha Yako. Kwamba Mungu Ana Uweza Wa Kunyamazisha Yote Kwa Baraka Zako Inakubidi Uwe Tayari Kusikiliza Na Kuwa Tayari Kuwakaribisha Ndani,” Rotimi aliandika kwenye chapisho la video yake.