Watu wa 'dreadlocks' msahau mbinguni - Yesu wa Tongaren

Yesu wa Tongaren aliradidi maneno hayo ambayo ni sawa na yale na mchungaji Ezekiel kuhusu ndoa na warembo wa rasta.

Muhtasari

• “Alisema siingi mbinguni kwa sababu niko na rasta,” Jahmby alisema akipakia picha ya pamoja na mchungaji huyo.

Yesu wa Bungoma asema watu wa rasta hawana nafasi mbinguni.
Yesu wa Bungoma asema watu wa rasta hawana nafasi mbinguni.
Image: Facebok

Yesu wa Tongaren, mchungaji kutoka kaunti ya Bungoma anayejitambulisha kama Yesu Kristo mtoto wa Mungu ambaye Wakristo wanapata hadithi zake kwenye Biblia anadai kwamba watu wanaofuga nywele za rasta hawana tikiti ya kuingia Mbinguni kwa ‘baba yake’.

Jamaa huyo ambaye amekuwa akizungumziwa pakubwa haswa msimu huu wa pasaka kuhusu uwezekano wa kusulubishwa kwake, alisema haya katika mahojiano na mwanahabari ambaye pia ni mkereketwa wa miziki ya Reggae na nywele za rasta, Fyah Mummah Jahmby Koikai.

Koikai alimtembelea nyumbani kwake huko Bungoma na kuwa na mazungumzo marefu naye ambapo jambo la kwanza ‘Yesu’ alisema baada ya kumuona shujaa huyo wa ugonjwa wa Endometriosis ni kwamba watu wenye nywele ndefu kama zake – dreadlocks hawawezi kuingia mbinguni.

Alisema siingi mbinguni kwa sababu niko na rasta,” Jahmby alisema akipakia picha ya pamoja na mchungaji huyo.

Maneno ya ‘Yesu’ yanaoana na yale ya mchungaji Ezekiel ambaye katika ibada yake kubwa wiki kadhaa zilizopita pia alizua mjadala mkubwa aliposema kuwa mwanamke mwenye nywele za rasta hawezi kudumu kwenye ndoa.

Yesu wa Tongaren amekuwa akitoa kauli tata kuhusu masuala mbalimbali, huku hivi majuzi akisema kuwa Wakristo hawafai kusherehekea pasaka mwezi Aprili, badala yake pasaka inafaa kufanyika mwezi wa Julai.

Yesu alisema kuwa Jahmby hangeweza kujinafasi katika nafasi ya watu wawili kutoka Nairobi ambao alisema kuwa ndio pekee watajiunga na msafara wake kwenda mbinguni, akisema kuwa kuzuizi kikubwa dhidi ya mtangazaji huyo na MC wa Reggae ni kutokana na kufuga dreadlocks.