Haya yamezidi,kujeni mnikamate-Muhubiri Ng'ang'a awathubutu polisi

Maoni yake yanakuja baada ya Mchungaji Ezekiel kukamatwa NA PLISI SIKU YA Alhamisi asubuhi.

Muhtasari
  • Kasisi huyo, mnamo Jumatano, alihojiwa kwa saa nyingi kwa madai kuwa kanisa lake linajihusisha na uchawi.
  • Mkuu wa Mkoa wa Pwani Rhodah Onyancha alisema kuna madai ya vifo vilivyoripotiwa katika eneo lake.
Mchungaji Ng'ang'a azungumzia maisha yake kabla ya kuokoka
Mchungaji Ng'ang'a azungumzia maisha yake kabla ya kuokoka
Image: Screengrab//SasaTV

Mwanzilishi wa Neno Evangelist James Ng'an'ga amethubutu serikali kumkamata.

Maoni yake yanakuja baada ya Mchungaji Ezekiel kukamatwa NA PLISI SIKU YA Alhamisi asubuhi.

Katika video ambayo inaenea kwenye mitandao ya kijamii, Mchungaji James Ng’ang’a anasikika akithubutu viongozi kumkamata ikiwa wanataka.

Haijabainika ni nini huenda kilichochea kauli yake.

“Mimi sijasoma lakini nyie mmesoma. Walakini, simu yangu inapokea pesa. Baada ya kumkamata mhubiri huyu hata wewe naomba nawe upate vivyo hivyo. Serikali ije kwa ajili yangu, hii sasa imezidi!” Anasema.

Mchungaji Ezekiel wa New Life Prayer Center  alikamatwa Alhamisi asubuhi. Alikamatwa kwa madai ya kufunzwa na umma.

Kasisi huyo, mnamo Jumatano, alihojiwa kwa saa nyingi kwa madai kuwa kanisa lake linajihusisha na uchawi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Rhodah Onyancha alisema kuna madai ya vifo vilivyoripotiwa katika eneo lake.

Mbunge wa Magarini kaunti ya Kilifi Harrison Kombe aliibua mapya kuhusu sakata linaloendelea kushika moto la mchungaji Paul Mackenzie kufuatia vifo vyenye utata vya makumi wa waumini wa kanisa lake huko Shakahola.

Kulingana na mbunge huyo, mchungaji Ezekiel Odero ambaye ametiwa mbaroni mapeni Alhamisi kufuatia za ndani zinazomhusisha na vitendo vya kupotosha kama vile vya Mackenzie, hahusiki kwa njia yoyote katika upotoshaji.

Kombe akizunumza asubuhi ya Alhamisi kwenye runinga ya Citizen alisema kwamba Odero ni mshirika wa kaunti kwa muda mrefu ambapo anatoa ushirikiano katika kufadhili masomo ya baadhi ya watoto wasiojiweza pamoja pia na kujenga vituo vya masomo na afya.

“Kwa muhtasari nimewahi kukutana naye, ni mshirika wa serikali ya kaunti, kuna mambo kadha wa kadha ambayo anafanya. Ndani ya Magarini anajenga zahanati ambapo ni kwa upande wa afya anajali na pia ameweza kutoa misaada ya chakula. Ni jambo ambalo tunalifurahia.”