"Mimi ndio niko!" Otile Brown amjibu mtu aliyemwambia siku hizi hafanyi vizuri kimuziki

“Siku za hivi karibuni hujakuwa ukifanya vizuri kaka, mashabiki wako tumechoka na wewe sana,” Derrick alimwambia.

Muhtasari

• “Tafadhali nakuomba rudi kwenye unyama wako. Ngoma baada ya ngoma halafu zote kali,” shabiki huyo aliwambia.

Otile Brown amjibu shabiki aliyesema amepoa sana
Otile Brown amjibu shabiki aliyesema amepoa sana
Image: Instagram

Msanii wa kizazi kipya nchini Kenya Otile Brown amemjibu shabiki aliyemnyooshea kidole akisema kwamba msanii huyo katika siku za hivi karibuni hafanyi vizuri katika sekta ya muziki.

Shqabiki huyo kwa jina Derrick Omwakwe kupitia ukurasa wa Instagram wa Otile Brown, alikuwa amepakia picha yake ikizunguka kwa njia ya video huku nyuma wimbo wake ukiimba na shabiki hakufurahishwa na wimbo huo.

Bila kuficha, alimwambia Otile kwamba katika siku za hivi karibuni nyimbo zake hazijakuwa na vaibu la kukosha kama awali, akisema kuwa yeye kama mwakilishi wa mashabiki wake, wamemtuma kumwambia kuwa hawana furaha na hali hiyo.

“Siku za hivi karibuni hujakuwa ukifanya vizuri kaka, mashabiki wako tumechoka na wewe sana,” Derrick alimwambia.

 Pia alimshauri kurudi kwenye mawanda yake ya awali na kujivika joho la mnyama hatari katika kutoa miziki ya kukosha.

“Tafadhali nakuomba rudi kwenye unyama wako. Ngoma baada ya ngoma halafu zote kali,” shabiki huyo aliwambia.

Lakini Otile kwa upole, alimwambia Derrick kwamba yeye tu ndiye yuko na atabaki kuwa Otile yule wa unyama mwingi kwenye muziki na kumtaka kusubiria vibao visivyo vya uzito wa mchezo.

“Otile anaweza kuwa mmoja tu. Usiwe na shaka na Otile huyo mmoja kwa sababu muziki mzuri bado unaendelea kukubaliwa,” Otile alijibu.

Msanii huyo juzi aligonga vichwa vya habari baada ya kumjibu shabiki wake rukuki aliyekuwa amejichora tattoo zake akionesha upendo kwake.

Mrembo huyo alisema kuwa baada ya kuchukua umauzi wa kuchora tattoo za Otile, marafiki zake wengi walimdhihaki wakisema hawezi kutana na Otile na kuwa alikuwa anaharibu muda wake tu kwa staa ambaye hata hawezi kumtambua.

Kwa kustaajabu, Otile aliona mahojiano hayo na kusema pindi atakaporudi kutoka London atahakikisha amekutana na mrembo huyo na kushiriki chakula cha jioni naye kama njia moja ya kukubali na kuonesha shukrani yake kwa shabiki wake.