Burna Boy afichua sababu kuu ya kuacha kucheza soka na kuzama kwenye muziki

Msanii huyo mshindi wa tuzo ya Grammy alifichua kwamba alikuwa anapenda soka sana na alikuwa anacheza kama golikipa.

Muhtasari

• "Sikujisikia muhimu sana. Sikuhisi tu kama nilihitajika hivyo. Nilihisi kama bila mimi timu bado itakuwa sawa" - Burna Boy.

Burna Boy afichua sababu za kuacha soka na kuzama kwenye muziki,
Burna Boy afichua sababu za kuacha soka na kuzama kwenye muziki,
Image: Instagram

Burna Boy hivi majuzi amewaruhusu mashabiki kujua jinsi alivyoachana na ndoto yake ya kuwa mwanasoka na kupata faraja katika muziki ambayo hatimaye ulimfikisha kwenye kilele cha maisha.

Mchezaji huyo anayejiita African Giant alidai nafasi yake wakati wa enzi zake za uchezaji walinda mlango lakini alifikiri ‘hakujiona kuwa muhimu’ kwa timu yake kwa sababu ‘kazi ya kipa anaganda langoni kama amekufa.’

Msanii huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy alitaja haya wakati wa mazungumzo na mwanahabari Julie Adenuga. Burna alisema kuwa hataki kutumia maisha yake yote kama golikipa na alidhani kuwa kikosi kingekuwa sawa bila yeye.

Alisema; “Napenda soka. Nilikuwa mzuri katika kucheza soka lakini jambo baya zaidi ni kwamba nilikuwa mzuri katika ulinda mlango. Ndio maana niliacha tu kwa sababu [kipa] alikuwa kama amekufa. Sikujisikia muhimu sana. Sikuhisi tu kama nilihitajika hivyo. Nilihisi kama bila mimi timu bado itakuwa sawa. Sitaki kutumia maisha yangu hivyo.”

Katika hadithi nyingine za Burna Boy, mwanamke aliyehudhuria tamasha la Burna Boy nchini Zimbabwe amemsihi mwimbaji huyo wa Nigeria amuoe baada ya video za maruweruwe yake wakati wa tukio la Burna Boy kusambaa mitandaoni.

Ellen Tsaura, sosholaiti wa Zimbabwe, alimwomba Burna Boy amchukue kama mke wake kwa sababu mpenzi wake alikuwa ameachana naye kwa sababu yake.

Kulingana na ripoti, Ellen alirusha vazi lake jeusi kwa Burna Boy wakati wa onyesho lake kwenye Belgravia Sports Club huko Harare, Zimbabwe, Juni 2022.

Mwanamke huyo mrembo alitweet habari kuhusu tamko lake la kumpenda mwanamuziki huyo wa Nigeria.

Ellen alifichua kuwa mwanamume wa hivi punde zaidi aliyemwacha alikuwa mpenzi wa tano kutengana naye kutokana na kisa hicho. Aliandika; "Niliachana na Boyfriend wangu wa 5 kwa sababu ya huyu @burnaboy lazima aje tu kunioa kwacho."