Diamond achafua hali ya hewa YouTube, mastaa wa Nigeria hawamfikii kwa takwimu

Hata hivyo, wasanii wengi kutoka Magharibi hawatilii maanani takwimu za YouTube kwa kile wanahisi kwamba mapato yake yako chini ikilinganishwa na majukwaa mengine.

Muhtasari

• Diamond mpaka sasa tangu aanze muziki takribani miaka Zaidi ya kumi iliyopita, ndiye msanii aliyetazawa Zaidi YouTube akiwa na views bilioni 2.14.

Diamond anguruma Afrika kote kimuziki.
Diamond anguruma Afrika kote kimuziki.
Image: Instagram

Mfamle wa miziki ya kizazi kipya ya Bongo Fleva kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amewaduwaza na kuwakanyaga vibaya wasanii kutoka Nigeria baada ya kuwapiku wote kwenye takwimu za muziki katika jukwaa la YouTube.

Msanii huyo ambaye alitua nchini Ujerumani kwa shoo yake kubwa Jumamosi hii alipakia takwimu mpya zinazowaonesha wasanii katika bara zima la Afrika na jinsi wanavyofanya kwenye jukwaa hilo.

Kulingana na takwimu hizo, Diamond ndiye msanii anayeshikilia usakani kwa maelfu ya wasanii kutoka mataifa yote ya Afrika kwa nyimbo zake kutazawa Zaidi na kutiririshwa kwenye jukwaa hilo la video.

Diamond mpaka sasa tangu aanze muziki takribani miaka Zaidi ya kumi iliyopita, ndiye msanii aliyetazawa Zaidi YouTube akiwa na views bilioni 2.14.

Wasanii wa Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanakuja katika nafasi zingine huku Burna Boy kutoka Nigeria akimkaribia Diamond kwa kutazamwa mara bilioni 2.05 kwenye YouTube.

Wizkid ametazamwa YouTube mara bilioni 1.67 huku Fally Ipupa, msanii wa Rhumba ya kizazi kipya kutoka DRC akiwa wa nne kwa takwimu za kutazamwa mara bilioni 1.40 na Davido anayezidi kutamba kwa albamu yake mpya ya Timeless akifunga tano bora kwa kutazamwa mara bilioni 1.29.

Diamond amekuwa akitamba kwenye jukwaa hilo la Video licha ya dhana kwamba wasanii wengi haswa kutoka Magharibi huwa hawazingatii sana takwimu zao kwenye YouTube kwa kile kinasemekana kuwa mapato kutoka jukwaa hilo bado yapo chini mno.

Kwa sababu hiyo, wasanii wengi sasa wanawekeza miziki yao katika majukwaa mengine kama Boomplay, Audiomac, Spotify na mengine ambayo aghalabu huwa hayachukui video na mapato yake ni ghali kuliko yale ya YouTube.