Rekodi za Dunia za Guinness ambazo zimewahivunjwa na Wakenya

Kenya inashikilia rekodi ya Dunia ya Guinness kwa ndege wengi zaidi walioonekana ndani ya saa 24.

Muhtasari

• Kenya inashikilia rekodi ya Dunia ya Guinness kwa ndege wengi zaidi walioonekana ndani ya saa 24, rekodi ambayo iliwekwa mnamo Novemba 1986.

• Kimani Ng'ang'a Maruge, alisababisha kufanywa  kwa filamu ya wanafunzi wa darasa la kwanza ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu mzee zaidi kuanza shule ya msingi.

Kuna baadhi ya rekodi za Dunia za Guinness ambazo zimewaivunjwa na wakenya katika ulingo mbalimbali.

Baadhi ya recordi zilizowai kuvunjwa na wakenya ni:

Rekodi ya idadi kubwa ya ndege katika saa 24

Kenya inashikilia rekodi ya Dunia ya Guinness kwa ndege wengi zaidi walioonekana ndani ya saa 24, rekodi ambayo iliwekwa mnamo Novemba 1986.

Rekodi hiyo iliwekwa na Wakenya Terry Stevenson, John Fanshawe na Andy Roberts katika siku ya pili ya tukio la kuwatazama ndege, Birdwatch Kenya mwaka wa 1986.

Mtu mzee zaidi kuanza shule ya msingi.

Kimani Ng'ang'a Maruge, alisababisha kufanywa kwa filamu ya wanafunzi wa darasa la kwanza ndiye anayeshikilia rekodi ya mtu mzee zaidi kuanza shule ya msingi.

Maruge alijiunga na Shule ya Msingi ya Kapkenduiyo mnamo Januari 12, 2004, akiwa na umri wa miaka 84.

Wakati wa kuandikishwa kwake katika shule hiyo yenye makao yake mjini Eldoret, wajukuu zake wawili walikuwa mbele yake katika shule hio hio.

Ziwa kubwa Zaidi kwenye jangwa

Ziwa Turkana, linalopatikaana upande wa  Kaskazini mwa Kenya linashikilia rekodi ya ziwa kubwa zaidi kwenye jangwa duniani.

Mwanariadha wa masafa marefi mwenye kasi zaidi

Mwanariadha wa Kenya Eliud Kipchoge ndiye anayeshikilia rekodi ya mbio za marathon zenye kasi zaidi, ushindi alioupata kwa saa 2:1:39 kwenye Berlin Marathon Septemba 16 2018.

Ushindi mara mingi na nchi moja kwa mfululizo wa IAAF World Cross Country Championships kwa wanadada.

Wanariadha wa kike wanashikilia recordi hio ya ushindi kwa mfululizo katika IAAF World Cross Country Championships.

Rekodi hii iliandikishwa kati ya 2009 na 2019.

Wanariadha hao walikuwa Florence Jebet Kiplagat (2009), Emily Chebet (2010 na 2013), Vivian Jepkemoi Cheruiyot (2011), Agnes Jebet Tirop (2015), Irene Cheptai (2017) na Hellen Obiri (2019).