"Hakuna mwanaume ameumbwa ku'cheat, msiamini kauli hiyo kutoka kuzimu!"

Mchungaji Okonkwo alimjibu vikali msanii 2baba Idibia baada ya kujitetea kwamba amezaa watoto 6 nje ya ndoa kwa sababu wanaume wote wameumbwa ku'cheat.

Muhtasari

• “Walakini, hii yote KAMWE sio kisingizio cha kudanganya na kumuumiza mtu unayedai kuwa unampenda, KUJIDHIBITI kwa neema ya Mungu ni jinsi ya kwenda,” Okonkwo.

mchungaji Okonkwo asema kuwa kauli ya kila mwanamume kucheat ni ya kuzimu.
mchungaji Okonkwo asema kuwa kauli ya kila mwanamume kucheat ni ya kuzimu.
Image: Twitter

Mchungaji mmoja kupitia jukwaa la Twitter amemjibu vikali msanii wa muda mrefu kutoka Nigeria, 2Baba Idibia baada ya kauli yake kwenye filamu ya Young Famous na African kwamba wanaume wote wameumbwa kuchepuka.

Akitumia anwani yake ya Twitter Kingsley Okonkwo alidokeza kuwa tabia ya kijinsia ya wanaume ni tofauti na ile ya wanawake kutokana na sababu mbalimbali, mojawapo ikiwa ni misukumo ya juu ya ngono ambayo wanaume huwa nayo.

Ingawa alikiri kwamba huenda wanaume wakashawishiwa zaidi kufanya ngono kuliko wanawake, alisema waziwazi kwamba hilo halihalalishi kufanya uasherati au kumdhuru mtu ambaye wanampenda kikweli.

Mchungaji huyo alisema kwamba hakuna kitu kama wanaume wote wameumbwa na mfumo wa kuchepuka ndani yao kwani kauli au wazo kama hilo si la Kimungu bali chimbuko lake ni jehamanu.

“Hakuna mwanamume aliyeumbwa kuchepuka, usiamini uwongo huo kutoka kuzimu. Hata hivyo inaonekana kuna uthibitisho kwamba wanaume wana uwezekano mkubwa wa kupata vishawishi vya ngono kuliko wanawake, BILA shaka wanawake pia hujaribiwa. Lakini kwa uwazi, uwezo wa kijinsia wa wanaume ni tofauti sana na wanawake hapa kuna sababu kadhaa,” aliandika.

Ili kutia mkazo na kiimbo Zaidi kwenye maelezo yake, mchungaji huyo alienda mbele na kutoa sababu kadhaa zinazofanya wanaume kuwa tofauti na wanawake, lakini sababu ambazo hazina msingi wowote wa kudhibitisha kwamba wanaume ni lazima wachepuke.

“Wanaume wana hamu kubwa ya kufanya mapenzi kuliko wanawake, wanaume wana kiwango kikubwa cha testosterone ambayo ni homoni ya ngono. Wanaume wanaweza kufurahia ngono bila uhusiano wowote wa kihisia, ndiyo maana ukahaba unafadhiliwa zaidi na wanaume. Wanaume wanachangamshwa macho, kwa hivyo kuwa mwanamume katika ulimwengu wa sasa ni jaribu la moja kwa moja kwa sababu mtazamo wako unashambuliwa kila siku.”

“Walakini, hii yote KAMWE sio kisingizio cha kudanganya na kumuumiza mtu unayedai kuwa unampenda, KUJIDHIBITI kwa neema ya Mungu ni jinsi ya kwenda,” Okonkwo alisema.

2Baba alitoa kauli hiyo kama njia ya kujitetea kwa kuzaa watoto 6 nje ya ndoa na wanawake wengine wawili kando na mke wake Annie Idibia.

Alikuwa akizungumza kwenye msimu wa pili wa filamu ya uhalisia kwenye Netflix ya Young, Famous & African.