'Ni muhimu kutafuta msaada,'Nyashinski awashauri mashabiki

Aliendelea kusema kwamba, wakati mwingine tunajikwaa na kuanguka.

Muhtasari
  • Aliongeza pia kuwa, kutafuta msaada kunasaidia kuinuka na kutoka kwake ambayo ni muhimu.
Nyashinski
Nyashinski
Image: Hisani

Mwimbaji na mtunzi mashuhuri wa Kenya Nyashinski ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwahimiza watu kutafuta usaidizi wanapokumbana na vikwazo na matatizon maishani.

Msanii huyo wa kibao maarufu cha  'Hapo tu' aliandika kama mbunifu akisisitiza kuwa ni sawa kutafuta msaada.

Aliendelea kusema kwamba, wakati mwingine tunajikwaa na kuanguka.

Aliongeza pia kuwa, kutafuta msaada kunasaidia kuinuka na kutoka kwake ambayo ni muhimu.

Pia alisema kwamba, kuna watu huko nje ambao wanataka kusaidia, kusikiliza na kuwa pale kwa ajili yako.

Alimalizia kwa kusema kwamba, ni lazima uchukue hatua ya kwanza.

Huu hapa ushauri wake aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram;

"Kama mbunifu, nasisitiza kwamba ni sawa kutafuta msaada ni muhimu. Sote tunajikwaa na kuanguka wakati mwingine, lakini ni jinsi tunavyoinuka na kujifunza kutoka kwake ndio muhimu. Kuna watu huko nje wanataka kusaidia. wanaotaka kukusikiliza na wanaotaka kuwa pale kwa ajili yako. Inakubidi tu kuchukua hatua ya kwanza na kufikia nje."

"Ni sawa kutafuta msaada" Mwimbaji Nyashinski Anawahimiza Watu Binafsi Wanapokutana na Vikwazo