Matukio katika Picha: Jinsi Boyz II Men walivyoteka Nairobi usiku wa Stanbic Yetu Festival

Tamasha la Stanbic Yetu liliandaliwa na kufadhiliwa na benki ya Stanbic kwa ushirikiano na kampuni ya Radio Africa.

Muhtasari

• Kundi la Boyz II Men linajumuisha Baritone Nathan Morris, Tenors Wanya Morris na Shawn Stockman.

 
• Kabla ya onyesho lao, mashabiki walifurahishwa na muziki kutoka kwa ma-DJ tofauti kuanzia saa kumi jioni.

Wanachama wa Boys II Men Shawn Stockman (kushoto) Wanya Morris, na Nathan Morris wakiwa jukwaani kwenye Tamasha la Stanbic Yetu katika bustani ya Uhuru mnamo Juni 10, 2023
Wanachama wa Boys II Men Shawn Stockman (kushoto) Wanya Morris, na Nathan Morris wakiwa jukwaani kwenye Tamasha la Stanbic Yetu katika bustani ya Uhuru mnamo Juni 10, 2023
Image: BRIAN SIMUYU// THE STAR

Usiku wa Jumamosi ya Juni 10, 2023 utasalia daima katika kumbukumbu za wengi waliohudhuria tamasha kuu la Stanbic Yetu lililofanyika katika uwanja wa Uhuru Gardens jijini Nairobi, shukrani zote kwa bendi ya Boyz II Men kutoka Marekani.

Wakongwe hao wa muziki aina ya R&N waliteka anga kwa utumbuizaji wao ambao uliwakosha wengi wa mashabiki waliohudhuria kiasi kwamba wengi hawakutaka wamalize kushuka ukumbini, na walipomaliza wengi walitamani angalau wangeendelea kwa saa zingine zaidi.

Licha ya mvua na hali ya hewa ya baridi, Wakenya walijitokeza kujionea tamasha lililokuwa likisubiriwa.

Tamasha la Stanbic Yetu liliandaliwa na kufadhiliwa na benki ya Stanbic kwa ushirikiano na kampuni ya Radio Africa.

Kundi la Boyz II Men linajumuisha Baritone Nathan Morris, Tenors Wanya Morris na Shawn Stockman.

Kabla ya onyesho lao, mashabiki walifurahishwa na muziki kutoka kwa ma-DJ tofauti kuanzia saa kumi jioni.

Walipanda jukwaani na umati wa watu ukaenda kwa fujo huku wakiimba pamoja na nyimbo zao.

Bendi ya Kenya Boy Sauti Sol ilichukua uongozi mwendo wa saa 7.30 usiku na kutumbuiza umati kabla ya Boyz II Men kupanda jukwaani.

Haya hapa ni baadhi ya matukio ambayo yaliweza kunaswa katika picha na wapiga picha wetu shupavu: