Jovial kurejea kufanya muziki baada ya mapumziko ya mwaka moja

Tangazo hili la Jovial linakuja siku chache tu baada ya kuachiliawimbo wake wa 'Don;t Give Up'.

Muhtasari

• Jovial alitangaza uamuzi wake wa kufanya muziki bila kushirikisha wasanii wengine baada ya mwaka moja wa mapumziko.

• Jovial alitangaza kwenye akaunti yake ya Instagram uamuzi wake wa kufanya muziki bila kushirikisha wasanii wengine baada ya mwaka moja wa mapumziko.

Image: INSTAGRAM/JOVIAL

Mwanamziki Juliet Miriam almaarufu Jovial, ametangaza uamuzi wake wa kurejea kufanya muziki wa kibinafsi baada ya kuchukua mwaka mmoja wa mapumziko.

Jovial alitangaza kwenye akaunti yake ya Instagram uamuzi wake wa kufanya muziki bila kushirikisha wasanii wengine baada ya mwaka moja wa mapumziko.

“Niko karibu kuachilia wimbo wangu wa kwanza kwa muda mfupi ujao” aliandika Jovial

Jovial aliongeza kuwa muda huo wa mapumziko ulimfaa na sasa anarejea na kuachilia wimbo mmoja baada ya nyingine.

“Haya sasa ni marathon... one after the other good music, good vibes”

Mwanamziki Jovial aliwachilia wimbo wake mpya hivi majuzi alimyomshirikisha Lexsil.

Wimbo huo uliibua gumzo mitandaoni baada ya muigizaji Bahati kuhusishwa kwenye wmbo huo. Bahati kuhusika kwenye video ya wimbo huo ulitokea baada ya yeye kutangaza kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Wanamitandao wengi walichukulia hatua hiyo ya bahati kuwa kama kutafuta kiki ili kuweza kuongeza umaarufu wa wimbo huo.

Kulingana na Jovial, Kurekodiwa kwa video ya wimbo huo "Don’t Give Up" ulimfanya akumbuke kifo cha baba yake mpendwa aliyeaga kutokana na kuugua ugonjwa wa saratani ya ubongo.

"Kurekodiwa kwa wimbo wa 'dontgiveup' ulikuwa mgumu, tulilia sana. kila mtu alikuwa na hadithi zake za kibinafsi na iliniumiza sana. Nilimpoteza baba yangu kwa saratani ya ubongo, jambo ambalo liliniuma sana, hata hadi leo nikikumbuka natokwa na machozi . Kuna siku mimi hukumbuka baba alishimdwa kumtambua mtu yeyote na hata mimi mtoto wake hakuweza kuongea nilipotaka aongee nami, ” alikumbuka.

Jovial alitangaza kwenye akaunti yake ya Instagram uamuzi wake wa kufanya muziki bila kushirikisha wasanii wengine baada ya mwaka moja wa mapumziko.