Msanii Jovial amtambulisha mpenzi wake kwa mara ya kwanza

Mwimbaji huyo alishiriki zaidi na video hiyo na nukuu inayosema Romeo & Juliet

Muhtasari
  • Video ilionyesha Jovial na mpenzi wa maisha yake walikuwa wakishiriki wakati mzuri, na alionekana akimpa shavu huku wote wakitabasamu wakitazamana kwa kamera.
Jovial
Image: HISANI

Mwimbaji mashuhuri wa Kenya Juliet Miriam Ayub almaarufu Jovial amemtambulisha mpenzi wake kwa mashabiki wake kwa mara ya kwanza kabisa.

Hit maker huyo wa 'Such Kinda Love' amefanya hivi leo, na hii ilikuwa kupitia chapisho kwenye akaunti yake ya Instagram ambapo ameshiriki kipande cha video wakiwa pamoja kwenye hadithi zake.

Video ilionyesha Jovial na mpenzi wa maisha yake walikuwa wakishiriki wakati mzuri, na alionekana akimpa shavu huku wote wakitabasamu wakitazamana kwa kamera.

Mwimbaji huyo alishiriki zaidi na video hiyo na nukuu inayosema Romeo & Juliet

Hata hivyo haikuwa wazi kama Romeo lilikuwa jina lake halisi, au alikuwa akilitumia tu kuhusiana na mchezo maarufu wa kimahaba ulioitwa Romeo na Juliet.

Katika chapisho lingine, mtayarishaji kibao wa 'Amor' aligusia uhusiano wake akisema:

"Chochote kizuri kinachotokea katika maisha yako UNASTAHILI!Ndivyo Mabwana wanavyofanya 🥰👌,"Aliandika Jovial.

Miezi 3 iliyopita Jovial alionyesha fahari yake kwa binti yake mdogo, Soilah.

Jovial alichapisha picha nzuri za malkia huyo mdogo kwenye Instastori zake na kuambatanisha na jumbe maalum kumhusu.

Chini ya baadhi ya picha alizochapisha, alidokeza kuhusu baadhi ya maelezo machache kuhusu baba ya bintiye asiyejulikana.

Binti yangu wa Kimasai," aliandika chini ya picha moja.

Kwa kauli yake, mwimbaji huyo mahiri ambaye ni Mluhya alidokeza kuwa baba wa mtoto wake ametokea katika jamii ya Maasai.

"Mix ya Mluhya na Maasai," aliandika kwenye picha nyingine.

Jovial aliendelea kufunguka upendo wake kwa bintiye na kueleza jinsi anavyonuia kumlinda kwa namna yoyote ile.

Pia alionekana kuwatahadharisha wapenzi wa baadaye wa binti huyo wake.

Miezi michache iliyopita, mwimbaji huyo wa kibao 'Jeraha' alidokeza kuhusu uhusiano mzuri kati yake na mzazi mwenzake asiyejulikana licha ya kutokuwa pamoja tena