Diamond awaacha mashabiki hoi akionekana na boxer pekee akiyumba kama mlevi

Diamond alikuwa kifua wazi huku mkononi ameshikilia simu yake na alionekana kuyumba kama mlevi aliyekosa dira.

Muhtasari

• Diamond alikuwa amealikwa kutumbuiza na katika video na picha za mitandaoni, alivishwa jezi ya Yanga na kutangazwa rasmi kuwa shabiki wao.

Diamond aonekana akiwa kifua wazi
Diamond aonekana akiwa kifua wazi
Image: INSTAGRAM

Msanii Diamond Platnumz amewaacha wengi katika hali ya utashi kutaka kujua alikuwa anafanya nini baada ya kuonekana akishuk kutoka kwa gari katikati ya barabara huku akiyumba kama mlevi na wakati huo huo amevalia kipensi pekee.

Mkurugenzi huyo wa kampuni ya Wasafi alipakia video hiyo kwenye Instagram yake bila kusema chochote na kuamua kukaa pembeni kuona mashabiki wake walikuwa wanasema nini kuhusu video hiyo.

Inaarifiwa kwamba msanii huyo alipakia video hiyo muda mchache baada ya kutoka katika tamasha la timu ya Yanga ambao walikuwa wanasherehekea ubingwa wa mataji matatu kwa msimu ambao umekamilika hivi majuzi.

Diamond alikuwa amealikwa kutumbuiza na katika video na picha za mitandaoni, alivishwa jezi ya Yanga na kutangazwa rasmi kuwa shabiki wao, licha ya muda mrefu kujulikana kuwa ni shabiki wa watani wa jadi, Simba SC.

Baada ya kushuka kwenye gari katikati ya barabara, Diamond alikuwa kifua wazi huku mkononi ameshikilia simu yake na alionekana kuyumba kama mlevi aliyekosa dira na kulifikia gari lililokuwa kando na kuliegemea kama nguzo.

Mashabiki wake walioona video hiyo walikuwa na haya ya kusema;

“Bro wear cloth u won’t die 🤣🤣🤣🤣 show off of six packs” Nastblaq alisema.

“If a poor man dresses like this,you go say dey be mad...But for celebrities it's fashion 🥺🥺” mwingine alisema.

“Boss, You will break record for most 8 packs in a body😂😂😂😂😂😂😂” Janemena alimwandikia.